Marais wote walipingwa ndani na nje ya chama, Samia sio wa kwanza

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Ukweli ulio wazi ni kuwa maraisi wote walipingwa vikali ndani na nje ya chama Wala Samia sio wa kwanza na hatakua wa mwisho.

Nyerere alipingwa,
Mwinyi alipingwa tena hadi ma Nyerere ambae alimpendekeza kuwa Rais.

Mkapa alipingwa
Kikwete alipingwa na hapa kwa kuwa ni miaka ya juzi wengi mnakumbuka, alipingwa kuanzia na spika Samwel Sitta hadi na Mawaziri wake.

Magufuli alipingwa na hii piaa tunakumbuka, Kinana, Makamba, Membe.

Mama Samia anapingwa, na Wala sio ajabu kabisa na ni lazima hiili liwepo.

Hakuna namna ambayo mama Samia atakubalika na wote ndani ya chama na Wala sio sababu yeye ni mwanamke au sijui ni dini gani la hasha. Anapingwa kwa kuwa binadamu kiasili ndivyo tulivyo hatuwezi kukupenda wote.
 
Ni kweli nakumbuka Nyoka wa makengeza Chenge,aliwahi kumwambia Jiwe anao uwezo wa kumukamata,lakini hakuwa na ubavu wa kumufunga.

Kuwa rais inahitaji ngozi ngumu.
 
Nyerere kaponea kupinduliwa mara nne (4) .

Tatizo watu wakiaddress issues kuna wengine wanawaona wasaliti.

Tunawekana sawa tu.

Watu wasiwe waoga sana kukosolewa.

Ni jambo la kawaida sana.
 
Back
Top Bottom