Marais Wenye Utajiri Zaidi Afrika

Martini Am

Member
Mar 7, 2016
9
6
Africa ni Bara la pili kwa idadi ya watu Duniani baada ya Bara la Asia. Wananchi wengi wa Kiafrika wanapitia maisha magumu kiasi cha wengine kuishia kupata mlo mmoja tu kwa siku. Haihitaji kuwa na Shahada ya Uchumi ili kuweza kufahamu kwamba nchi nchi nyingi za Kiafrika bado zina uchumi wa hali chini.

Lakini amini usiamini, viongozi wengi wa Kiafrika wana utajiri wa kutisha.

Tukianzia juu kwenda chini, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, anakamata namba 8 katika orodha hiyo. Rais Robert Mugabe ana umri wa miaka 92 na anapanga kuendelea kukaa madarakani kwa kipindi kingine cha uongozi ambacho kitamfanya atawale mpaka akiwa na miaka 98. Rais Mugabe ambae amekaa madarakani tangu mwaka Disemba 22 mwaka 1987, ana utajiri unaozidi dollar za kimarekani milio 10. Rais Mugabe anatamani kuendelea kukusanya fedha kwani ameshawaambia wanaotamani kumrithi ni vyema wakawa na subra zaidi kwani yeye bado yupo yupo sana Duniani na ataendelea kuwa Rais.

Namba saba kwenye orodha ya Marais wenye Ukwasi ni Rais Idris Deby wan chi ya Chad. Rais Deby amekaa madarakani tangu mwaka 1990 , madaraka ambayo aliyapata kwa njia ya uasi. Kwa mujibu wa jarida la Celebrity Net worth,… utajiri wa Rais Deby ni zaidi ya Dollar za Kimarekani milioni 50.

Nambari sita mkuu wa Taifa la Swaziland..Hapa tunamzungumzia mfalme Mswati wa Tatu (III) ..Achilia mbali utitiri wa Wanawake anaomiliki, Mfalme mswati ana zaidi ya dollar milioni 100 kama utajiri wake binafsi. Mfalme mswati anasifika kwa matumizi…wakati wanachi wa Swaziland wanalia njaa, mwaka 2014 wake zake 13, walitumia dolla milioni 6 kwa ajili ya shopping zao za kawaida tu. Inaaminika mfalme Mswati anamiliki magari mengi ya kifahari amabyo hata hivyo, amepiga marufuku mtu yeyote kupiga picha mgari yake.

Namba 5 ni Rais Paul Biya wa Cameroon. Inonekana kwamba marais waliokaa mdarakani muda mrefu wana utajiri mkubwa zaidi. Mwaka 2009, gazeti la Rue 89 la Ufaransa, liliandika kwamba safari za Rais wa Cameroon, zilikuwa ghali zaidi kuliko safari z Rais mwingine yeyote Ulimwenguni. HATA Rais wa marekani hafui dafu. Kwa sasa utajiri wake unakadiriwa kuvuka dolla za kimarekani milioni 200.

Namba 4 ni jirani yetu, ndugu yetu, mwanachama mwenzetu wa katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Muigai Jomo Kenyatta, ana utajiri unaozidi dolla za kimarekani million 500. Familia ya kina Kenyatta ina miliki sehemu kubwa ya ardhi ya Kenya na hivyo kuwa kati ya sababu zinazochangia utajiri wake. Utajiri wa Uhuru pia unatokana na vyanzo vingine vya mapato kama kiwanda cha kusindika maziwa cha Brookside Dairies, kampuni ya masuala ya habari iiitwayo Mediamax, hoteli za kitaalii ziitwazo Heritage Hotels.

Taedoro Obiang Nguema Mbasongo , Rais wa Guinea ya Ikweta, anshika namba 3 akiwa na utajiri unaozidi dolla million 600 za kimarekani. Huyu ndio Rais aliekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi hapa Afrika, aliingia madarakani mwaka 1979 baada ya kumpindua baba yake mdogo kabisaaa, Marehemu Francisco Nguema.

Namba 2 ni mfalme wa morocco, Mfalme Mohamed wa 6, ambae ana utajiri wa takriban dollar za kimarekani bilioni 2.1. Mohamed wa 6 alikaa madarakani tangu mwaka 199 baada ya kifo cha babayake, Hayati mfalme Hassan wa 2.

Na sasa nakujuza Rais ambae ana utajiri kuliko kiongozi mwingine yoyote barani Afrika. Huyo ni Rais Josee Eduardo Dos Santos wa Angola. Wakati anayemfuatia ana utajiri wa dola za kimarekani bilioni 2.1, jarida la Cabinda online linaeleza kwamba Bwana Josee ana utajiri wa zaidi ya dolla bilioni 20 za kimarekani. Familia ya Rais Jose Eduardo Dos Santos inanuka fedha kwani binti yake Isabel Dos Santosa, anatajwa kuwa mwanamke tajiri zaidi Afrika akiwa na utajiri wad olla bilioni 3.8; hiyo ina maana kwamba hakuna Rais yeyote Afrika anaekaribia utajiri wa Binti wa Rais wa Angola. Upo hapo?

Hao ndio marais wenye ukwasi zaidi barani Afrika, amabo wanadhihirisha namna ambavyo dunia imejaa maajabu na matajiri wa kutisha.
 
Kuna Kiongozi mmoja kwa safari moja ya wiki moja tu alibeba dollar milioni tano, kwanini hayupo kwenye orodha.
 
Hivi ukisema 10$ million ni sawa na billion 20 point kadhaa za kitanzania...hivi kwa haraka haraka unadhani Mzee wa Msoga hana huo mkwanja??? Ukipiga hesabu ya utajiri wa mtoto wake utajiridhisha kwamba Mzee hata namba tatu angeingizwa kwenye list
 
Habari zenu wakuu leo ningependa niwape list chache ya maraisi wenye mtonyo au ukwasi wa kutosha wa AFRICA

1 : Rais wa Angola ana utajiri wa Usd 20bn.

2 : Uhuru Kenyatta ana utajiri wa Usd 500milion

3: Paul Bier wa Cameroon ana utajiri wa Usd 200milion

4: mfalme mswat anautajiri wa Usd 100milion

5: raisi wa chad anautajiri wa Usd 50milion

6:raisi mugabe wa zimbabwe anautajiri wa Usd 10milion

Tanzania hatupo kwenye list hii kama wapo wengine unao wajua waongeze hapo chini tafadhari ili tujifunze kitu ila katika list yangu rais wa Angola ndiye anayeongoza kuwa na pesa nyingi Usd 20bn.
 
Wote hao waliingia Madarakani wakiwa ni Maskini.

Kasoro Uhuru, utajiri wake ni wa Kurithi(wa familia)

Tutarajie na Sizonje kuwa kwenye list.
 
Habari ya kutunga blaza.....

Haiwezekani namba 1 akawa ana 20 Billion anaemfatia ana 0.5 Billion

Kwa sisi ma Engineer tunasema "Your comparison is void"
 
Hizi data huenda sio sahihi, zingelikuwa na usahihi naona hawa wote kasoro wa Angola wanaweza kuwa vibarua wa mmoja ambaye hujamuweka!
 
Habari ya kutunga blaza.....

Haiwezekani namba 1 akawa ana 20 Billion anaemfatia ana 0.5 Billion

Kwa sisi ma Engineer tunasema "Your comparison is void"
Amewaruka hawa,
1.Mohamed VI wa Morroco 2.1bn
2.Teodoro Obiang Nguema Mbasogo-Equatorial Guinea-$600m
 
Nadhani kuna mtu hapo kufikia 2020 atakuwa ni bilionaire namba Moja Africa nzima maana yeye toka ameingia kajiwekea mapesa mingi mno maana ukijiuliza yale mapesa ya ajira mpya kayatia mfukoni,mapension,madaraja ya watumishi yote katia mfukoni. Hapo asiwe billionaire?. mwafaaa
 
Back
Top Bottom