Marafiki

Husna Muba

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
14,524
Reaction score
44,585
Marafiki wawili *(Elias na Ben)* walikuwa wanatembea mtaani, akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.

Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:

*Ben:* Mwanaume. Muone yule mrembo amenirushia busu

*Elias:* Kidume, tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..

_(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)_

*Ben:* Mwanaume yule mwanamke ameniita!

*Elias:* Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.

*Ben:* Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu

*Elias:* Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kule _(akihisi kutotiliwa maanani)_

_(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla, wakasikia mlio WA gari getini)_ .. [emoji344][emoji344]

*Lady:* _(akiangalia kupitia dirishani, Akasema Kwa Kutaharuki)_
*Oooh! Yule ni mume wangu!!*

*Ben:* Mama yangu !
Nipo matatani, Kweli!!?

*Lady:* Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo

*(akimuonyesha lundo la nguo)*

_(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)_

_(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)_

*Ben:* Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???

*Elias:* Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha, *Nilizifua Mimi Juzi!!*
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

*Fundisho la Stori,

"Mtu mwenye uzoefu akiongea jambo ni vyema kumsikiliza na sio kumpuuza"
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…