Old Member (Retired)
JF-Expert Member
- Sep 29, 2012
- 3,402
- 1,618
Hii imemkuta ndugu yangu wa karibu aliyekuwa akifanyakazi ofisi fulani hapa nchini, Baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha miaka kadhaa alikuwa amejikusanya weeeee pamoja na biashara zake akajenga kajumba kake ka ghorofa mbili bila kumwambia mtu mwingine zaidi ya wanafamilia na ndugu wa karibu.
Alipokuwa anataka kuhamia akaamua ndipo kwenda kuifanyia maombi nyumba yako akawaalika watu kadhaa wakiwemo marafiki na jamaa wengine (BILA KUMSAHAU RAFIKI WA DAMU, TOKA NITOKE, SHIDA YA MMOJA SHIDA MWINGINE, RAFIKI TOKA SHULE YA MSINGI CHUO KIKUU MPAKA KAZINI).
Siku chache baada ya maombezi ya nyumba yake akapokea simu kutoka kwa waandishi wa habari wakisema wanaomba aeleze ametoa wapi hela za kujenga nyumba ile?
Jamaa akawa anashangaa kwamba hawa watu wamekosea au? akawauliza mnajua mnaongea na nani wakamjibu tunaongea na.....unaishi maeneo ya .... unafanyakazi ofisi ya?
Jamaa akaishia kushangaa tu, kwamba imekuaje. Ikabidi awakatie simu, wakapiga tena hakupokea kabisa.
Wiki inayofuata wakaguzi (auditors) wakaja kukagua mahesabu pale ofisini, kama unavyojua kibongo bongo auditors wakikushtukiza bila huwezi ukakutwa msafi kirahisi rahisi.
Jamaa akakutwa na mapungufu katika hesabu za zale wakakuguzi, muda mchache akashtakiwa kwa kutumia ofisi kwa maslahi yake binafsi. Siku zote jamaa anajiuliza hili swala limefikiaje hapa?
KUMBUKA katika kila hatua anayokumbana nayo ye alikuwa akienda kwa rafiki yake kumuomba ushauri na rafiki kweli anamshauri na jamaa anamueleza mbinu zake za kukabiliana na hiyo kesi.
Ubaya ni kwamba, kila plan yake ilikuwa inavuja na hafanikiwi na katika kipindi hicho chote alikuwa kasimamishwa kazini.
Katika kuhakikisha kesi yake hiyo inaisha ndugu huyu aliuza gari zake mbili na kwa kutumia njia anazozijua yeye kabla ya kesi kuisha mmoja wa waandishi wa habari,....... na ....... walimwambia huyo ambaye upo nae ndiye anayekuzunguka, taarifa zote yeye ndiye ameleta na siri zako zote ulizokuwa unampa alikuwa anazileta kwetu.
Mpaka leo hii ndugu huyu hana rafiki mwingine zaidi Mungu.
KWELI MARAFIKI NI WANAFIKI TU
MCHUNGUZI HURU