Marafiki wa Lowassa waja na staili mpya

Marafiki wa Lowassa waja na staili mpya

mwinukai

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Posts
1,447
Reaction score
630
Moshi. Mbunge wa Moshi Vijijini na Mjumbe wa Nec ya CCM, Dk Cyrill Chami, amewaomba walimu zaidi ya 2,700 wamuombee Waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili ‘ndoto' yake iweze kutimia.

Wakati Dk. Chami akiwaomba walimu hao, mtandao wa marafiki wa Lowassa Kanda ya Kaskazini, juzi walikuja na staili mpya ya kumshawishi Mbunge huyo wa Monduli agombee nafasi ya Urais.

Staili hiyo mpya imekuja wakati CCM ikiwa imempiga ‘stopu' kuendelea na utaratibu wake wa kupokea makundi ya watu wanaomshawishi kugombea urais na yeye (Lowassa) kuridhia na kuwaomba wananchi wasubiri maelekezo ya CCM.

Marafiki hao ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, walikwenda kitengo cha damu salama Kanda ya Kaskazini kuchangia damu kama njia ya kutambua na kuenzi upendo wa Lowassa.

Tukio hilo la wanafunzi hao kwenda katika kitengo hicho, kilitanguliwa na tukio la mkutano mkuu wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) ya Walimu Moshi Vijijini kufanya mkutano wao mkuu. Katika mkutano huo, Dk Chami aliyekuwa mgeni rasmi, aliwaambia amekwenda pale akiwa na salamu kutoka kwa Lowassa kwamba anawapenda sana walimu. "Anasema anawapenda na anawakumbuka sana na anawaomba mmuombee ili ndoto yake na ile safari yake (bila kuitaja) itimie," alisema Dk Chami na walimu hao kulipuka kwa vigelegele.

Katika tukio la uchangiaji wa damu, wanafunzi zaidi ya 100 wa vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, walitumia tukio hilo kumuunga mkono Lowassa wakimsihi atangaze nia ya kuwania Urais 2015.

Mratibu wa marafiki wa Lowassa, Noel Nnko, alisema wanafunzi hao wameamua kuchangia damu kumuunga mkono kada huyo kwa vile wao hawana uwezo wa kutoa fedha za kuchangia fomu.

Chanzo:
Mwananchi
 
Ndoto aote lowasa walimu ndio wamuombe ili hiyo ndoto iweze kutimia!!!

Ujinga mwingine unalemea sana.
 
Lowassa anashawishiwa kwa lipi, wakati inajulikana wazi kwamba Urais anautaka kwa udi na uvumba, tangu mwaka 1995? Maigizo mengine bhanaaaaa!!!!!!
 
Mbona anamashaka sana??? kama anaamini yeye ni bora atulie asubiri wakati wa kampeni aombe kura watu watampa. ila anavyojihami sasa anazidi kunifanya nimdisqualify
 
by the way: Hata yule rais wa chama cha soka aliyepo madarakani kwa sasa aliwaaminisha watu kuwa anaweza, matokeo yake kila mtu ameona. Kwani kuwasaidia wananchi lazima uwe na cheo kikubwa??. aaaah .. not always you need a big tittle to help citizens
 
Anadumisha fani yake aliosomea huyo. Hana jipya
 
Pole yenu nyie nyote ambao hadi muda bado mnaamini huko CCM bado kuna mtu aliebaikia kuweza kuongoza Taifa hili.....wengine cc Tumeachana na ndoto hizo miaka mingi Poleni sana ila mjue kuendelea kujifanya vipofu nakuendelea kuchagua CCM mnaangamiza hii NCHI kwa mikono yenu wenyewe
 
Ngoma ikivuma sana,mwishowe hupasuka......!
 
Lowassa anatumia nguvu nyingi kuaminisha uma kama anapendwa...Cyrill chami nae anamtetea lowassa kwa sababu ameahidiwa kurudi kundini iwapo atapita... Hapa unakuja kuona wote wanaomtetea lowassa huwa wanatetea interest zao na matumbo yao!!!

Hakuna mtu timamu anayeweza kutoa mchango wa damu yake kisa lowassa jambazi kuu la kwenye Richmond
 
Faiza FOXY alisema eti Lowassa ana Parkinson's disease!! Hii sheria mpya ikianza kutumika huyu shori lazima atakwenda kunyea ndoo!!
 
Lowassa must be the most popular person in Tanzania. CCM wakitaka kubaini hili wapeleke jina la Membe, Lowassa, Wasira, January Makamba, Pinda, Mwigulu na Mwandosya kwenye NEC tujue nani zaidi.
 
Lowassa mbona ana kiherehere kama anafaa mbona ni debe tupu ambalo haliachi kutika?

Chema hujiuza na kibaya kama hiki cha Lowassa hujitembeza
 
lini fisadi akachukuwa lini? anapendwa kwa ufisadi wake na kwa kutoa michango ambayo ina sura nzuri huku ni hongo, fisadi bwana
 
Hivi hizo ndoto za lowahasa kila siku anaota hata mchana?
 
Lowassa ni Fisadi mkuu nchi hii ndiyo maana alijiuzulu, Hivyo ufisadi ni ugonjwa mbaya sana kuliko hata huo alionao wa Kutetemeka. Aachane na mambo ya urais kwani bado ni mchafu sana, Nchi yetu itakuwa rehani tukiendelea ku entertain haya maigizo ya Lowassa
 
Back
Top Bottom