Mara ya mwisho Liverpool kuchukua ubingwa wa Uingereza mambo yalikuwa hivi

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Wahusika wa Liverpool nimeikuta hii sehemu sijui ukweli wake ukoje.

Mara ya mwisho Liverpool kuchukua ubingwa wa Uingereza ilikuwa siku ya Jumamosi, Aprili 28, 1990 baada ya kuifunga QPR goli 2-1.

ANC ilikuwa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini.

NCCR Mageuzi lilikuwa vuguvugu la kutaka mabadiliko ya katiba Tanzania.

Rais wa Marekani alikuwa George Bush mkubwa.

Soda moja ilikuwa shilingi 40/=

Tanzania Bara ilikuwa na mikoa 20.

Stendi ya mabasi ya Mikoani ilikuwa Kisutu na Mnazi Mmoja.

Palipo na Ubalozi wa Marekani palikuwa Drive Inn Cinema.

Kasper Schmeichel hakuwa amezaliwa lakini mwaka jana kachukua ubingwa na Leicester City.

Jose Mourinho hakuwa ameanza kuwa kocha lakini katwaa ubingwa huo mara 3.

De Gea hakuwa amezaliwa lakini katwaa ubingwa huo.

Noti ya juu kabisa Tanzania ilikuwa shilingi 1000/= na shilingi 10/= ilikuwa ya noti.

Rais mstaafu Benjamin Mkapa alikuwa waziri, JK alikuwa naibu waziri na JPM alikuwa mwalimu wa sekondari. Wote hao wameshakuwa marais.

Kumbi maarufu za burudani Dar zilikuwa La Prima, Bahama Mama na Mbowe. Na moja ya bendi maarufu ilikuwa Bima Lee Orchestra.

Msemo maarufu ulikuwa 'la kupalama la kuchumpa' na msichana aliitwa 'kishtobe'.

Sanduku la Posta ndo ilikuwa kitu cha kurahisisha mawasiliano na duniani tulikuwa na penpal friends.

Sir Alex Ferguson alikuwa na miaka 3 tu toka awe kocha wa Man United. Ameshastaafu baada ya miaka 27 na sasa ni miaka minne tangu astaafu.

Man United ilikuwa imeshatwaa ubingwa wa ligi mara 7 tu na Liverpool mara 18. Lakini leo hii Man United keshatwaa mara 20 na Liverpool bado hizo hizo 18.

Sehemu kubwa ya Ubungo ilikuwa pori na Sinza bado kulikuwa na mashamba ya mpunga.

Viwanda maarufu vya nguo vilikuwa Sunguratex na Urafiki. KTM Mbagala haikuwepo. Kwanza Mbagala yenyewe ilikuwa porini kabisa.

Timu maarufu kwenye ligi ya Tanzania ukiachia Simba na Yanga, zilikuwa Pilsner, Sigara, Tukuyu Stars, Lipuli, Ushirika Moshi, Pamba, Nyota Nyekundu, Milambo, Reli, MECCO, Coastal Union, Pan African, Ujenzi Rukwa na RTC Kagera.

Marijani Rajab alikuwa bado hai.

Diamond Platinumz hakuwa ameanza hata shule ya vidudu.

Kiongozi aliyekuwa akiogopwa duniani alikuwa Saddam Hussein.

Stori maarufu Tanzania zilikuwa za Willy Gamba. Jarida maarufu zaidi lilikuwa Sani la kina Bawji na Nico ye Mbhago na Tanzania Film la Faraji H H Katalambula.

Mchoraji maarufu zaidi alikuwa John Mathias Kaduma.

Kimsingi, ndo ivo.
 
Naweka historia sawa. Ilipoanza kutumia VAR uingereza ndo liverpool ilipochukua kombe
 
Back
Top Bottom