Mara ya Mwisho kwa Rais Kuhudhuria Mdahalo/Mkutano na Wanachuo na akaruhusu Maswali

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Marais wa nchi za wenzetu hufanya hivyo. na si jambo baya kuiga. swali langu mara ya mwisho ilikuwa lini rais alikutana na wanafunzi wa chuo akafanya nao mdahalo au akahutubia na mwishoni akaruhusu wamuulize maswali naye akayajibu pasipo shida.
1. naomba nipewe jina la rais huyo
2. jina la chuo
3. mwaka aliohudhuria
4. mada au maswali aliyoulizwa.

nawasilisha mada.
 
Umenikumbusha miaka ile ya 90 enzi hizo ndio mzee wa Kiraracha kahama CCM kujiunga na upinzani (NCCR). Enzi hizo midahalo pale UDSM ikiwa hot kweli na pale Nkrumah palikuwa na sharti moja; kwamba pale ni lazima midahalo na speech zote ziwe kwa lugha ya Malkia.

Ha ha ha! Bwana we! Siku hiyo kaingia Mh; ukumbi umefurika; kila mmoja hadi maprofesa wana hamu ya kumsikiliza Mzee wa Kiraracha - kumbuka ulikuwa ni uthubutu wa aina yake; kujiondoa CCM, tena Mwalimu akiwa hai; siku chache baada ya Kolimba kufariki; haikuwa jambo la masikhara - ni kuweka rehani uhai wako.

Ilibidi kanuni "zitenguliwe" fasta kwa kile kilichodaiwa "ili mazungumzo yalete ladha na mtiririko mzuri"; na kwa mhemuko uliokuwepo siku ile hakuna namna ungeweza kuzuia hili. Ni kwa jinsi hii Mzee wa Kiraracha aliweza kuteta na wanazuoni.
 
Naonaga kina Kagame wanaenda Havard au Oxford wanatoa lecture na wanapigwa maswali.
Hapa baada ya Nyerere sijui kama kuna mwingine.
 
Naonaga kina Kagame wanaenda Havard au Oxford wanatoa lecture na wanapigwa maswali.
Hapa baada ya Nyerere sijui kama kuna mwingine.
... na Kagame ni miongoni mwa maraisi wasiojua darasani kunafananaje along with Jacob Zuma, na wengine kadhaa Afrika.
 
Back
Top Bottom