Mara ya mwisho Azam fc kuifunga Simba kwenye Ligi kuu

Pabloz

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
1,818
9,180
Mara ya mwisho Azam FC kumfunga mnyama kwenye ligi kuu Tanzania Bara ilikuwa Tarehe 28 January, 2017.

FT| Simba SC 0-1 Azam FC
77'|⚽ John Bocco

Kikosi Cha Simba kwenye hiyo mechi:
1. Agyei 2. Bokungu 3. Zimbwe Jr 4. Banda 5. Mwanjale 6. Mkude ©️ 7. Mnyate 8. Ndemla 9. Luizio 10. Athanas 11. Mzamiru SUBS: Manyika jr, Lufunga, Vincent, Mavugo, Kichuya, Ajib, Coster.
Kocha Mkuu: Omog

Kikosi cha Azam kwenye mechi:
1. A. Manula 2. Gadiel Michael 3. Erasto Nyoni 4. Yakubu 5. A. Morris 6. H. Mao 7. Mahundi 8. Stephan 9. Bocco ©️ 10. Domayo 11. Singano
SUBS: Metacha, Mwantika, Kheri, M. Yahya, Masoud,. Yahaya. M, Chilunda.
Kocha Mkuu:Aristica Cioaba

Kuna Mambo mengi yametokea ndani ya hii miaka minne amayo Azam hajapata ushindi dhidi ya Simba.
1. John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni wameenda Simba SC.

2. Simba SC imeshinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara mara 3 mfululizo.

3. Kocha wa Azam aliyeshinda hiyo mechi, Aristica Cioaba aliondoka, akarudi Azam na ameondoka tena.

4. Msimu huo wa 2016/17, Bingwa alikuwa Yanga na alichukua ubingwa kwa tofauti ya magoli dhidi ya Simba baada ya kulingana alama na Simba na ulikuwa msimu wa mwisho Yanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.

5. Gadiel Michael alienda Yanga na sasa yupo Simba.

Wewe unakumbuka tukio gani lililotokea ndani ya hii miaka minne?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom