Mara: Bweni la Shule ya Sekondari Bumangi Wilaya ya Butiama lateketea kwa moto

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Wanafunzi wa kidato cha tano sita na tatu wa Shule ya Sekondari Bumangi Wilaya ya Butiama mkoani Mara wamenusurika kifo baada ya bweni kuteketea kwa moto muda mfupi baada ya wanafunzi hao kuondoka bwenini na kwenda kusali ambapo mali zao zote zimeteketea.

gtrvf.jpg
 
Tuanze kuwalaum Tanesco ikiwa chanzo cha moto kitathibitika kuwa ni tanesco.kwa nini shule zinaungua kwa moto wa umeme? tuanzie hapo kwanza
 
Lakini sijaona (I stand to be corrected) ya mtu binafsi ikikumbwa na hili janga. Naona nyingi zinamilikiwa na taasisi za kidini
Ngoja tuone mwisho wake, halafu kama umegundua wanatime ile muda ambao bwenini hamna wanafunzi ndo wanachoma (naona hawana lengo la kuuwa watoto wa watu)
 
Hivi katika main switches za hizi shule hawana kile kifaa Circuit breaker ambacho huzima umeme automatically kinapo detect electric shocks au unusual/excess usages ya umeme!? Au wana wiring gani za umeme hizi shule? Au watu wanachoma na mishumaa hizi bweni? Wajuzi wa umeme mtusaidie tafadhari...
 
Hali inaogopesha sana.

Yaani haimaliziki wiki, Mabweni, au Madarasa yanaungua.

Je kuna hujuma inayofanyika?

Au kuna agenda ya siri inayoendelea?

Kulikoni!
 
Kila wakati shule zimekua zikiteketea kwa moto Chakushangaza hakuna sheria iliyopitishwa kuhakikisha kila shule inakua na zile fire extinguisher ambazo zingeokoa gharama za miundo mbinu inayoteketea +vifaa vya Hao wanafunzi ,tumeona moto katika magari ya mafuta yakileta madhara, moto katika misitu na mashamba sasa katika mashule ,nishauri elimu itolewe kwa Jamii ikiwezekana kila nyumba iwe na fire extinguisher na majiko/mitungi ya gesi yawekwe nyumba tofauti ,pia elimu itolewe kwa jamii hasa mashuleni na katika jamii kiujumla lengo kujikinga, kuokoa na kuzuiya janga hili.
 
Dah! Wadogo zetu wanaoishi mabwenini wataishi kwa woga. Kila siku mabweni yanaungua.
 
Wanafunzi wa kidato cha tano sita na tatu wa Shule ya Sekondari Bumangi Wilaya ya Butiama mkoani Mara wamenusurika kifo baada ya bweni kuteketea kwa moto muda mfupi baada ya wanafunzi hao kuondoka bwenini na kwenda kusali ambapo mali zao zote zimeteketea.

View attachment 1633780
Mkuu huu ni wakati sasa wa kuwa na uhitaji wa kuwa na FIRE suppression system pamoja na fire fighting systems katika shule.Tusijifanye hatuoni tatizo.Ni wakati sasa wa kuwa na mfumo mzuri wa firfigting katika shule.Tukiendelea hivi tutapoteza watoto wengi sana.
 
Kila wakati shule zimekua zikiteketea kwa moto Chakushangaza hakuna sheria iliyopitishwa kuhakikisha kila shule inakua na zile fire extinguisher ambazo zingeokoa gharama za miundo mbinu inayoteketea +vifaa vya Hao wanafunzi ,tumeona moto katika magari ya mafuta yakileta madhara, moto katika misitu na mashamba sasa katika mashule ,nishauri elimu itolewe kwa Jamii ikiwezekana kila nyumba iwe na fire extinguisher na majiko/mitungi ya gesi yawekwe nyumba tofauti ,pia elimu itolewe kwa jamii hasa mashuleni na katika jamii kiujumla lengo kujikinga, kuokoa na kuzuiya janga hili.

sheria mbona ipo kitambo sana ,huwa hawakagui wanasubiri janga litokee ndio waende kuuliza 1.mna fire extinguisher ? 2.mlizifanyia service muda gani ?
ni kama ule utaratibu wa kufanya service ya school bus zote kila mwisho wa mwezi sasa hivi umekufa ila likitokea la kutokea mtu atabanwa
 
Juzi kati shule ya Wasichana ya Loreto inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza iliteketea kwa moto. Sasa moto umehamia mkoani Mara.

Hivi kwanini hadi sasa mamlaka zetu zimeshindwa kubaini chanzo cha mioto hii (sina uhakika kama moto una wingi) ?
 
Kila wakati shule zimekua zikiteketea kwa moto Chakushangaza hakuna sheria iliyopitishwa kuhakikisha kila shule inakua na zile fire extinguisher ambazo zingeokoa gharama za miundo mbinu inayoteketea +vifaa vya Hao wanafunzi ,tumeona moto katika magari ya mafuta yakileta madhara, moto katika misitu na mashamba sasa katika mashule ,nishauri elimu itolewe kwa Jamii ikiwezekana kila nyumba iwe na fire extinguisher na majiko/mitungi ya gesi yawekwe nyumba tofauti ,pia elimu itolewe kwa jamii hasa mashuleni na katika jamii kiujumla lengo kujikinga, kuokoa na kuzuiya janga hili.
Sheria ipo. Sema hujui. Kila shule au taasisi zinatakiwa kuwa na vifaa vya kuzimia moto.
 
Back
Top Bottom