Mapunye: Fahamu kuhusu chanzo, tiba na athari zake kwa ngozi yako

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209

Wanangu wameugua mapunye (vibarango) na nimetumia dawa nyingi bado naona hawaponi. Nitumie dawa gani ambayo haishindwi?

SAME CASES:
---
---

UGONJWA WA MAPUNYE
Mapunye ni aina ya magonjwa ambayo hushambulia keratini zinazopatikana katika nywele hasa za kichwani. Fangasi aina ya Dermatophites husababisha ugonjwa huu.

USAMBAAJI
Kusambaa kwaugonjwa huu ni pamoja na Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtu mmoja hususan pale ambapo mmoja wa watumiaji hao ana maambukizi ya vimelea vya fangasi hao.

-Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari -Kushirikiana mavazi aina ya kofia na mtu aliyekwisha pata maambukizi hayo.

WANAOWEZA KUUPATA UGONJWA HUU
  • Watu wachafu.
  • Wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri
  • Wanaoshirikiana vifaa vya kufanya usafi wa mwili zikiwamo taulo
  • Wanaofanya kazi zinazohusisha uwekaji vichwa kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu
  • Wale ambao tayari wana fangasi za kichwani kwani ni rahisi kwa fangasi hao kujirudia.
  • Wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea
  • Wasiojikausha vichwa baada ya kuoga au kufanya usafi wa kichwa
  • Watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kingaikiwamo kisukari.
  • Wale wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibayotiki) kwa muda mrefu
  • Watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa balehe.

DALILI ZA UGONJWA
Mara nyingi aina hii ya fangasi hugundulika kwa macho hasa kwenye maeneo ambayo fangasi hao wapo kwa wingi. Kwa kutazama ngozi ya sehemu ya kichwa iliyoathirika na maambukizi ya fangasi hao, utaweza kuona madhara yanayokukabili.

MATIBABU
Mara nyingi mapunye hutibika kwa dawa za kutibu fangasi za kupaka ambazo hutibu mapunye na kuyaponyesha kabisa bila kuhitaji kutumia dawa za kumeza. Hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika.

Jinsi ya kujikinga
Kuna mbinu mbalimbali za kujilinda usipatwe na fangasi:
  • Hakikisha mwili wako hasa kichwani yanabaki na ukavu muda wote
  • Osha nguo, taulo na mashuka kuhakikisha fangasi wanaondolewa
  • Epuka kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele hasa kama hakuna namna ya kuvisafisha na dawa maalum ya kuua vimelea kabla hujatumia
  • Epuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanya usafi wa mwili kama mataulo. Kama kazi yako inahusisha ukaaji wa muda mrefu kwenye maji basi hakikisha unakausha mwili hasa sehemu za kichwa au uweke dawa ya kuzuia fangasi kwenye maji hayo.

MICHANGO YA WADAU:
---

---
---
 
Ni ugonjwa wa ngozi na kwa kuanzia anza na usafi wa mwili ikiwa ni pamoja na kuondoa nywele zote; tumia sabuni zakuogea zenye tiba kwa ngozi kama detol ya maji na usipende kufuga nywele ndefu kwa sasa mpaka ukipona wakti huo huo maji yako ya kuoga jaribu kuyachemsha kabla hujayatumia unaweza kuyaacha yapoe ama ukayaoga ya moto!

kwa watoto chunguza pia viyu wanavyotumia kwa usafi kama ni vya kushare na hsa vifaa vinavyotumika kunyolea ikiwa wanyoa nywele.
 
Pole kwa tatizo hilo, jitahid kuwanyoa nywele hao vijana wako halafu kuna dawa ya mba ya kijani ina xstics za spirit inavikausha within 1 week!ol the bect!
 
Pamoja na usafi kama kutumia mafuta yenye sulphur, kunyoa nywele na kutumia sabuni ya dawa , jaribu kuwapa dawa za minyoo; minyoo mara nyingine husabaisha ngozi kuharibika kwa kuota vipele.
 
Wanangu wameugua mapunye (vibarango) na nimetumia dawa nyingi bado naona hawaponi. Nitumie dawa gani ambayo HAISHINDWI?
Wapeleke hospitali maana that is fungal disease na kuna fungus wengine wapo kwenye damu, hivo ukiwanyoa na kupaka dawa wanaisha na kurudi tena haraka wanahitaji kupima damu na kuchomwa sindano ili kuwaua hawa wadudu kwenye damu!!
 
Wakuu kwa wale wataalamu naomba endapo kuna dawa kiboko ya kuponyesha mapunye yanayojitokeza kichwani. Nina watoto mmoja miaka 4 na mwingine miaka 9. Wanasumbuliwa sana; nimejaribu dawa nyingi za kupaka pamoja na sabuni (medicated soaps) lakini kupona hakupo! Msaada tafadhali.
 
Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.
 
Nadhani pia huwa inakuwa kwenye umri, maana nikiwa mtoto nakumbuka nilipataga nikawa sipendi kabisa na nilijaribu dawa nyingi ikiwepo moja inayoitwa B-Tex ambayo ilinisaidia sijui kama bado ipo.

Nakushauri wapeleke watoto kwa daktari wa ngozi coz inamuumiza sana mtoto kisaikolojia anapoteza hata uwezo wa kujiamini mbele ya wenzako, at that age mtoto ameshaanza kujitambua.

Pole
 
Mshubiri Mwitu au Aloe Vera kwa jina lingine. Ponda paka kichwani kila siku mara mbili asubuhi na usiku.
 
Ahsante FaizaFoxy. Dozi hii ni ya siku ngapi au hadi nione dalili za kupona? Nifahamishe tafadhali.

Hiyo ni mpaka upone na kupona huanza immediately na huchukuwa siku tatu mpaka kumi inategemea na uwingi wa hayo mapunye, utashangaa.
 
Pia, uwe unawanyoa nywele hao watoto angalau kila baada ya wiki mbili. itasaidia kuona kama kuna sehemu sehemu zingine zimepata upele na kama ni dawa inapakika vema kabisa (evenly).
 
Mpwa wapeleke wakachek damu zao pima full b pictur usiogope hii ni mwanzo nakama unaogopa nenda hata na housgirl akupe company

Fuata ushauri wa hapo juu na ikiwezekana chukua na wangu chukua maji weka kwenye sufuria kadogo kichwa chao kinaenea weka nusu ya vinegar kama maji then wainamishe vichwa kwa dk 15
mara tatu kwa siku njoo rudi usafiri na didy bure sichaji mtu
 
Habari wadau?
Mimi nina mtoto wa mwaka mmoja ambaye amepata punye eneo la kisogoni,punye hilo kalipata tangu akiwa na miezi 9,nimempeleka hospitali tukaandikiwa dawa atumie lakini bado halijapona,pia nimempa syrup ya minyoo last week lakini tatizo liko palepale,naomba msaada tafadhali.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Pole sana Jaribu hizi dawa moja kati ya hizo Dawa tatu hapo chini:

(1) Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga Msuguwe limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe maji ya Uvuguvugu halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

(2) (Fenugreek) kwa lugha ya kiswahili inaitwa Uwatu. Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya Uwatu (fenugreek) unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote.

(3) Mshubiri Mwitu au Aloe Vera kwa jina lingine. Ponda paka kichwani kila siku mara mbili asubuhi na usiku. Tumia Dawa mojawapo sio zote tafadhali kisha utpe feedback.
 
Kunadawa in aitwa "Dawa ya Mba", niya maji inarangi ya kijani, unampaka kwakutumia pamba sehemu iliyoathiriwa.
NOTE
Siyo ya kunywa.
Kidogo inaleta maumivu.
 
Nina dawa nlipewaga hospital ni ya unga wa njano, ina tibu kila kitu cha ngozi, vipele, chunusi, mkanda wa jeshi,f angasi, mapunye, makovu etc siijui inaitwaje kitaalamu,ila unaichanganya na mafuta ya mgando kisha unapka sehemu hucka haipt wiki pamepona..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…