Mapungufu ya Radio Times Fm

nndondo

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
1,251
895
Jamani wiki hii nzima nimekua nikisikiliza radio hii inayorusha matangazo yake toka kawe beach na kupata mshangao wa hali ya juu. Vipindi nilivyosikia ni pamoja na Campus na twende sijui ambapo kuna wazungumzaji notably mdada na moca.

Ni aibu kuwa sana kuona radio hii iliyvo na watangazaji mediocres, pamoja ya kwamba watangazaji wengi wa hizi radio station ni unschooled, kitendo cha vijana hawa kujifanya wajuaji katika kucheza na lugha wasioiweza ndio kiliniacha hoi. watangazaji wana uelewa mdogo sana juu ya hoja wanazozileta, kwa uhakika hawajiandai wala kuzisoma. kwa mfano leo moca na huyo mwenzake walileta habari muhimu ya wizi uliofanywa na walinzi wa Suma JKT, Pale UDOM.

Kwa bahati mbaya huyo dada hakujipanga kujua nini hasa anachotaka kukipeleka kwa wasikilizaji wake, mimi nilifikiri issue ilikua je, inakuaje jeshi la kujenga taifa likawa na walinzi hatarishi kwa taifa?

To me that was the issue, na labda angeenda kuangalia mfumo mzima (kama angekua na akili kidogo tu ya kuandaa topic yake) wa recruitment, staffing, remuneration, background information, placement, na labda hata list of clients wao.

Mbaya zaidi ni pale ndugu moca kama vile katoka kuzima alipokua akiingilia kujaribu kujiuliza maswali ya kipumbavu huku akionekana mtupu kabisa kwenye kujua hiyo Suma JKT ni nini. Akajaribu kujifanya anatania kuelezea computer CPU ni nini ooh my godness foolish kabisa. Kwa bahati mbaya sana sina mawasiliano na uongozi wa hiki kituo mbali na kwamba najua ni watoto wa smart guy Richard Nyaulawa, naomba sana tena sana msitishe mara moja ujinga unaofanywa kwenye kipindi hiki

The university show, a mediocre
Now we come to the campus bash, ambapo kulionekana kuwa na watangazaji kibao akiwemo masanja, jerry koto, mwakasungula etc, one may wonder hivi story kubwa ya vyuo ni wazee wa ATM na sasa namna ambavyo hao watangazaji wanavyosema, kuvuta sauti na kingereza kibovu unakata tamaa kabisa na elimu na vijana wa nchi hii, actually walli onyesha kabisa uduni wa ellimu ya chuo.

Mijadala yao ni haina maana na inafaa kujadiliwa na vijana wa mtaani wasioenda shule, kipindi kina jina zuri, delivery very very very poor, haija brand kabisa hujui walitaka kusema nini. it is a missed opportunity tunashindwa kabisa kutumia vyombo hivi vinavyoendeshwa kwa garama kubwa kuleta any impact au kuendelea kupata wadhamini.

Ninaamin huyo dr mwaka na hao tigo kama wako makini hawatarusha matangazo yao hapo. Nataka kumpa 10 mtangazaji Dina nafikiri alikua na kipindi cha taarabu, na tangazo la huyo dr wa utasa, she is professional and i google her to find that she is experienced, hawa wageni wanaojazwa studio ni vizuri wakafundishwa kazi na kujifunza toka kwa wenzao, vipindi vingi vya radio hiii na nyingine za namna hii ni kelele, vurugu, nonsense kila mtu akijaribu kumuiga mkude simba, hapana, tafuteni na nyie signature yenu hiyo ya hapa kazi tu, ni nzuri, play around it using intelligent people, huyo moca try him somewhere else, au apewe script if he has to sit in the studio, hafai kabisa kwa live.

ushauri wa bure
Kwa watanganzaji wote wa radio, remember sio kila mtangazaji anaweza kuwa jovial na aka crack jokes, unless yuko very sure na audience yako, kwa hawa hapa hawaijui audience yao hivyo hawawezi ku click na sisi, 2nd, you can only crack a joke in the language you are comfortable with, sio hicho kiingereza kibovu ajabu, wengi wenu bado hamjaweza kuunganisha maneno mawili, you are still on a single word syllabu sio mbaya, chomekea tu lakini usithubutu kutaka kutueleza kitu kwa kizungu.

Beside sisi wote tunaelewa kiswahili, ushauri, fuatilia kazi za Rebeka Mwaleko, za huko nyuma, she never worried about kizungu cheku kichafu and yet vipindi vyake vyote kikiwemo kile cha jifunze kiswahili were exemplary, she was natural and was capitalising on what she was able to do and did it well, leo hii yuko majuu,
 
yah umetetea vizur sana hoja yako, am sure watafikishiwa hii complain na kuifanyia kazi. good job
 
Ila na wewe si ungeeka paragraph unaanza na 1) topic sentence 2)supportive sentence 3) evidence/example 4) connecting sentence

Inarahisisha kusoma mzee, good message but a little bit an acquaintance in writing skills

Hope they wont disdain your observation, thanks
 
Hii radio ilikuwa na watangazaji wazuri sana ila kuanzia mwaka jana wengi wamekimbia....jabiry na gadna wsmeenda efm , kuna mwingine kaenda clouds...mtangazaji mwenyr uwrzo ni dida wa taarabu wengine ni vimeo tupu kichwani iq ndogo sana sijui ata uongozi unajiskiaje kuw na watangazaji dizain ile...sikiliza efm wapo serious mkuu alafu napenda wame base local content .
 
that field now is almost terrorized by the bunch of pumpkins ni makanjanja tu hamna kitu hapo.
 
Back
Top Bottom