Mapungufu makubwa ya muswada

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,859
1,301
Kwa kuwa niko mbali na siwezi kuwahi dsm au dodoma, na kwa kuwa spika amekataa kuwaruhusu wabunge kuja kwenye majimbo yao ili tuujadili huo muswada, nimeona nitoe maoni yangu katika forum hii.
Najarbu kubreak huo muswada katika vipande vipande ili niweze kuuattach; kwasasa pata hiyo.
MAPUNGUFU YA MUSWADA
Interpretation sect 3
-Constitutional organs means the president, the constituent assembly or the national assembly.
Lakini the president ni nani? – not defined
constituent assembly ni kitu gani – not defined
the national assembly.ni kitu gani – not defined
Bila kueleza vitu hivi mjanja yeyote anaweza kuchomeka chombo chochote, mfano bunge kuwa ndilo constituent assembly!

Ni muhimu pia kudefine president ni nani kwani tutaona huko mbele alivyopewa madaraka makubwa Kwa mfano isemwe tu kwamba the president means the president of Tanzania
Part III
Hapa tunaona madaraka makubwa ya president juu ya hii commission
Sec 5 The presideny may,………….establish a commission to examine……
Hapa kuna tatizo moja kubwa kisheria; neno ‘may’ halimlazimishi huyo president kufanya hivyo tofauti na kama ingetumika neno ‘shall’. Halafu ile comma imewekwa baada ya may ndiyo sababu ya kusema kuwa hiyo may inahusu ku-establish hiyo commission. Kama comma ingewekwa kabla ya may, basi ingehusu consultations with the president of Zanzibar.
Kwa hiyo president ndiye anaanzisha hii commission
Sec 6 (1) President ndiye atateua wajumbe wote wa hiyo commission
Sec 6 (2) ni vigezo vya kuchagua wajumbe, hapa vimetajwa vigezo (criteria), lakini kigezo (e) president amepewa madaraka ya kuamua vigezo vingine vyovyote atavyoona vinafaa – bila masharti yoyote wala kuulizwa na yeyote!
Sec 6(3) kinawaondoa baadhi ya watu kuwa wajumbe wa commission
Sec 6(3) (a)…a councilor or a leader of a political party. Yaani viongozi wa vyama vya siasa hawawezi kuchaguliwa kuwa wajumbe. Lakini huyu president (kama ndiye president of Tanzania) ni kiongozi wa chama cha siasa. Ina maana kiongozi wa chama kimoja cha siasa amepewa mamlaka makubwa ambayo viongozi wenzake wa vyama vingine vya siasa wamenyimwa! Kwa hiyo ataweka mbele maslahi ya chama chake (Labda hapa ndipo inakuja shida ya kuwa na president ambaye ni sehemu ya executive)

Sec 8 (1) The terms of reference shall be issued by the president….president huyo huyo ndiye ataipa hiyo commission hadidu za rejea yaani ataiambia nini cha kufanya! Na kwenye ya sec 8(3) hayo atakayowambia kufanya yanapewa nguvu ya kisheria. Maana yake president atatunga sheria yeye mwenyewe!
Ukisoma sec 9(1) (c) utaona kuwa hii commission ndiyo itaandika katiba ya awali. Je si ni wazi kuwa katiba hiyo itaandikwa kwa matakwa ya aliyewateua na kuwapa majukumu?
Kifungu cha 9 (2) kimeifunga mikono commission juu ya (a) muungano wa Tanganyika na Zanzibar na (c) urais. Je kama wananchi wanataka muungano wa kuwa nchi na serikali moja, maoni hayo yatashughulikiwa na nani? Je kama wanataka muungano uvunjike kila nchi ijitawale kivyake – maoni hayo yatachukuliwa na nani?
Kuhusu urais, watu wana mapendekezo ya kutaka rais asiwe sehemu ya serikali – wasemee wapi?

Sec 13 Commission itakuwa na secretariat ambayo katibu wake atateuliwa na president!
Sec 16 Commssion itapeleka ripoti yake kwa president ambaye atampatia nakala rais wa Zanzibar.
President atamuagiza waziri wa sheria na katiba kupeleka constitutional bill kwenye constituent assembly ambayo kama nilivyosema hapo awali haikuwa defined.
Sasa madaraka zaidi yanayokaribia labda ya kimungu yapo kwenye hiyo constituet assembly. Nimeona niscan hizo sections:


Kwa hiyo madaraka yote juu ya hiyo assembly yapo kwa persident hadi kutangaza majina ya wajumbe aliowachagua kwenye gazeti; Hiyo ni sec 21.
Sec 22 (1) madaraka ya hiyo assembly hayajali kuwapo kwa madaraka kama hayo kwa bunge.
Yaani hapa president amepewa madaraka ya kuteua chombo na wajumbe wake chenye kutumia madaraka yake notwithstanding kwamba madaraka kama hayo yapo kwa bunge!
Madudu yasiyokubalika yako mengi. Labda nimalizie kwa keleza kuwa kifungu cha 26 kinaipatia tume ta uchaguzi kuendesha kura ya maoni. Ni tume hii hii inayolalamikiwa kuwa siyo huru. Na swali litakaloulizwa ni la kujibu ndiyo au hapana.
Kifungu cha 28(2) kinasema kuwa kampeni ya kura ya maoni itaendeshwa na commission, Ni hiyo hiyo iliyoteuliwa na president, ni commission hiyo hiyo iliyodraft katiba, halafu ni hiyo hiyo peke yake inapiga kampeni! Vyama vya siasa havitaruhusiwa kuendesha kampeni, na mtu yeyoye atakayekampeni ambaye siyo mwana-commission atahukiwa kifungo bila faini.
NAFASI YA MWANANCHI AMBAYE NDIYE ANATAKIWA AAMUE NCHI YAKE ITAKAVYOENDESHWA, AMEACHWA NA KUTOA MAONI (SI MAAMUZI) NA MWISHO KUHUBIRIWA SEMA NDIYO! Ni vigumu kwa commssion kukampeni kuwa hiyo katiba iliyoandikwa na wao wenyewe ikataliwe!
Je hayo ndiyo tuliyolilia?
 
Hiyo bill haipatikani katika website yoyote? Nisaidie.

Mkuu Kashaija hiyo bill mbona imeshabandikwa kwenye thread kibao hapa jamvini jibidishe kidogo utaiona.

Kamakabuzi yote uliyoongea yana-make sense lakini cha kushangaza serikali ama ni kipofu au wameamua kuwa vipofu wasione.
Baya zaidi wameamua kuwa viziwi wasisikie kile wananchi wanataka juu ya huo mswada.
Asubuhi ya leo nimemsikia Chikawe (sikumbuki ni waziri wa nini) anasema wananchi wana imani na judgement ya Rais wao ndio maana walimchagua.
Hivi kama baba yangu tu hana ultimate decision katika maswala yangu iweje nimpe mtu baki (Rais) kunifanyia maamuzi. Hata tukikubali kwamba Rais alichaguliwa na wananchi ile 38% (ya kuchakachua) iliyomkataa matakwa yake yatawakilishwa na nani??

Inatia hasira pale watu wazima wanapogoma kutambua ukweli ulio dhahiri.
 
Hiyo bill haipatikani katika website yoyote? Nisaidie.
pole mkuu, fuata link hii: www.jamiiforums.com/katiba/tanzania-consitutional-review-bill-2011.pdf,
kama hiyo link ikikataa fuata njia ndefu ifuatayo:
www.jamiiforums.com/members/candid-scope.html hapo itafungua profile ya candid scope, kwenye hiyo profile click kwenye find all strated threads; hapo zitafunguka threads zote alizoazisha huyo member. Tafuta thread inayoitwa muswada sheria ya mapitio ya ... hapo utapata link ya moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom