Kanyunyu
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 335
- 495
Habari wana Jamvi
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI Wiki iliyopita imeanza kuhamisha Walimu kutoka idara ya Sekondari kwenda kufundisha Shule za msingi ili kukabiliana na upungufu wa Walimu. Utaratibu huu wa kuhamisha Walimu Umekuwa ni wa kienyeji sana na usiozingatia taratibu na HAKI za mtumishi husika. Mapungufu makubwa ni kama ifuatavyo,
1. Mwalimu husika anakabidhiwa barua ya uhamisho na kuambiwa Nenda kuripoti haraka Shule ya msingi uliyopangwa na uanze Kazi Mara Moja , hapa hakuna utaratibu wa kuwaandaa Walimu kisaikolojia (semina) kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kufundisha Shule za msingi.
2. Hakuna utaratibu wa kuwasafirisha Watumishi kutoka Kituo cha awali kwenda Kituo kipya (hakuna malipo ya nauli na Mizigo) mtumishi atajihamisha Kwa gharama Zake.
3. Hakuna malipo ya usubumbufu
4. Hakuna malipo ya Posho ya kujikimu
5. Hakuna nyumba za Watumishi, mtumishi atajua mwenyewe sehemu ya kukaa anakohamishiwa Kituo kipya. Mishahara kidogo afu nyumba upange Kwa mshahara huohuo mdogo. Huu ni uonevu wa kiwango cha juu sana.
Serikali hii ya awamu ya Tano haina huruma na Watumishi hawa ambao maslahi ya mishahara ni midogo sana na hawajapandishwa madaraja Kwa miaka 3 sasa kutokana na tamko la Rais Magufuli kuzuia Watumishi kupandishwa mishahara na madaraja.
Serikali hii ya wanyonge acheni kutesa Watumishi wa umma, HAKI na WAJIBU ndiyo msingi Mkuu wa Kazi.
Rais Magufuli amekuwa akisisitiza Watumishi wasikubali kuhamishwa bila kulipwa na ni marufuku kumhamisha mtumishi bila kuwa na bajeti ya kumlipa. Hivyo hawa Walimu wana HAKI ya kugomea uhamisho huu mpaka walipwe ?
Kazi kwenu wenye HAKI na nchi hii.