Abeto Malakoti
Senior Member
- Feb 7, 2018
- 122
- 234
Hati ya kiapo (affidavit) ya mashtaka ya kikatiba (Petition) Ado Shahibu ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii hususani JF, whatsapp, facebook n.k ina mapungufu kadhaa ya kisheria kama ifuatavyo;
Kwanza, hati ya kiapo kisheria ni ushahidi wa maandishi katika kesi za kikatiba, rejea section 12 ya the Basic Rights and Duties Enforcement Act. Haya ya 3 ya hati ya kiapo imeegemea kwenye press release ya katibu mkuu kiongozi, Kijazi kama udhibitisho wa uteuzi wa Dr. Kilangi kuwa mwanasheria mkuu ambapo huu ni udhaifu kwa sababu udhibitisho wa uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali wenye hadhi ya juu wa kiushahidi (high evedential standard) unapatika kwenye gazeti la serikali. Uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali unatangazwa kwenye gazeti la serikali na huu ndo ushahidi wenye hadhi ya juu kisheria na sio press release ya katibu mkuu kiongozi. Hivyo, Ado alipashwa kuambatanisha gazeti la serikali ambalo lilichapisha uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali kama taarifa rasmi ya kisheria kwa umma wa watanzania.
Pili, kwenye Haya ya 14 Ado kwa kutumia maneno "to the best of my personal knowledge" ametoa viashiria vya lazima (necessary implications) kuwa hana uhakika kama Dr. Kilangi aliwahi kufanya kazi serikalini zaidi ya nafasi ya mwenyekiti wa PURA na kusahau kuwa haya maneno ni ushahidi kamili maana yanasemwa chini ya kiapo na pia amesahau kuwa wajibu wa kudhibitisha (onus of proof) swala la kuwa Dr. Kilangi hajawahi fanya kazi serikalini kwa muda wa miaka 15 ni wajibu wake yeye mleta mashtaka (petitioner) mahakamani, he who alleges must prove, kisheria Dr. Kilangi hana wajibu wa kudhibitisha swala hili ni petitioner (Ado) ndo ana wajibu wa kudhibitisha. Hili kurekebisha kosa hili, Ado itabidi afanya maombi ambayo kisheria yanaitwa application for discovery au application for interrogatories.
Tatu, ushahidi wa kudhibitisha Roll Number na tarehe ya Dr. Kilangi kupata uwakili ni taarifa alizotoa kwenye website ya Tanganyika Law Society, nyaraka hizi zina thamani ndogo ya kiushahidi (low evedential value). Ado alipashwa kuandika barua kwa Msajiri wa mahakama kuu kuomba na kupatiwa taarifa rasmi za Dr. Kilangi kuhusu Roll Number na tarehe ya Dr. Kilangi kupata uwakili, mimi nimewahi kufanya hivi mara kadhaa na kufanikiwa kubatilisha kesi ya wakili ambaye ana leseni ya uwakili (practicing certificate) au kushuhudia kiapo kwa kughushi (backdate) kabla ya kuwa wakili. Taarifa rasmi kutoka kwa msajiri wa mahakama kuu ambaye ni custodian wa taarifa za mawakili ndo ina thamani ya juu ya kiushahidi kuliko taarifa za kuokoteza kutoka kwenye tovuti ya TLS.
Nne, ni makosa ya uchapaji kwenye ukrasa wa mwisho wa hati ya kiapo ambao badala ya kuandika "the president of united republic of Tanzania" ameandika "the president of united renational electoral commission". Haya makosa ya uchapaji ni madogo hayana madhara kisheria, wanasheria wanasema ni curable errors.
Kikupata fursa ya kuona Originating Summons ambayo inasindikizwa na hati ya kiapo ili niweze kuona mapungufu ambayo yako kwenye hiyo Originating Summons, hivyo ninatoa wito kwa comrade Ndugu Ado pia asambaze Originating Summons kwenye mitandao ya kijamii kama JF, whatsapp na facebook tuweze kuisoma na kuikosoa hili kumuepusha na mapingamizi ya awali (preliminary objections) ya wanasheria wa serikali hususani Wakili Mwandamizi Kadushi, mbobezi katika maswala haya ya mapingamizi ya awali.
Ni hayo tu Comrade Ndugu Ado Shaibu