Sio maprofesa tu, kwa mfumo wa serikali uliopo na uadilifu wa mashaka wa baadhi ya viongozi ndani ya CCM na jinsi ya viongozi walio wengi wanavyopata uongozi kwa kutumia rushwa ni vigumu kupata viongozi wasafi! In short ni rahisi mtu msafi kujiingiza kwenye vitendo vya ufisadi akishajiunga kwenye siasa za CCM na serikali kwa sababu kubwa moja. Viongozi wengi wasio waadilifu ndani CCM au serikalini wanaamini kwa kusupport chama tawala, tayari unakuwa juu ya kanuni, taratibu na sheria za nchi na vyombo vyake kama polisi, usalama wa taifa au TRA. So huu ulevi uwafumba macho, masikio na pua. Hii humfanya kiongozi yoyote bila kujali kiwango chake cha elimu kufanya vitendo vya kifisadi akiwa ndani ya ofisi za umma. Bado mchakato wa katiba mpya unaendelea, hivyo sisi kama watanzania bila kujali itikadi za vyama vyetu vya kisiasa na makundi mengine ya kijamii kuhakikisha katiba inaweka misingi thabiti ya uwajibikaji kwa viongozi wa umma. Hii ni pamoja kueleza kwa uwazi na uthibiti miiko na maadili ya viongozi wa umma.