Mapquest bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapquest bongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyani Ngabu, Jun 29, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Jun 29, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna huduma yoyote inayofanana na mapquest Tanzania?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,597
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama itakuwepo, maana kuna mitaa mingi haina majina halafu pale uhindini wahindi wamebadilisha majina ya mitaa mingi na kuweka majina ya kihindi bila hata ya kuwa na kibali cha jiji.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jun 29, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I thought so...Shukrani Bubu.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mitaa hipi tena BAK
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,597
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280

  Majina ya mitaa Dar yabadilishwa kinyemela

  Na Happy Wamanyamba

  BAADHI ya mitaa maarufu katikati ya Jiji la Dar es Salaam imebadilishwa majina, huku uongozi wa Jiji na Manispaa ya Ilala ukidai kutokuwa na taarifa za mtu aliyebadili majina hayo.

  Baadhi ya mitaa iliyobadilishwa majina ni Mtaa wa Kisutu ambao hivi sasa unajulikana kwa jina la Mtaa wa Pramukh Swami, na mwingine ni mtaa uliopo jirani na mitaa ya Jamhuri na Zanaki, ambao sasa umebadilishwa jina na kuitwa Mtaa wa Hazrat Abbas (A.S).

  Viongozi wa Jiji na Manispaa ya Ilala ambao walizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wote walikwepa kuzungumzia suala, wakidai kuwa si wahusika.

  Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Alhaji Adam Kimbisa , alipoulizwa kuhusu taratibu zilizotumika katika kubadilisha majina ya mitaa hiyo, alisema wahusika wakuu ni Meya wa Manispaa ya Ilala na si yeye.

  "Waulize mameya wa manispaa husika wao ndio wanajua wanatumia taratibu gani, kwani kila manispaa inataratibu zake, hivyo mimi sijui ni taratibu gani zimetumika katika kubadili majina hayo," alisema Kimbisa.

  Mbali ya Kimbisa, Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, ambako mitaa imebadilishwa majina na kupewa majina ya wageni, naye alikwepa kuzungumzia mabadiliko hayo.

  "Ni mitaa gani imebadilishwa? Mbona mimi siijui? Hata hivyo taratibu zilizotumika katika kubadili majina ya mitaa sizijui, labda watafute madiwani na wenyeviti wa mitaa husika ili waweze kueleza sababu za kubadilisha majina ya mitaa hiyo, ila mimi sifahamu," alisema Jumaa.

  Kubadilishwa kwa mitaa hiyo kiholela kumekuwa kukisababishia baadhi ya watu, hasa wageni, kupata usumbufu, kutokana na majina yaliyozoeleka kubadilishwa.

  Kwa kawaida, majina ya mitaa hubadilishwa na manispaa zinazohusika, na mara kwa mara, majina ya watu maarufu katika taifa au hata maeneo ya kihistoria na mambo kama hayo, hutumika kupata majina ya mitaa.
   
 6. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ha ha ha!What have you been thinking?
   
 7. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,822
  Likes Received: 20,805
  Trophy Points: 280
  ama kweli SHAMBA LA BIBI........hadi mitaa inabadilishwa watu hawana habari.......
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jun 29, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha..I know riiiight

  Well, I'll blame it on the Mary Jane....
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,597
  Likes Received: 82,153
  Trophy Points: 280
  Wako busy wanafanya ufisadi.
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Google Maps ndo inacome closest kwa bongo.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jun 30, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Basi ipo kazi, kwani wahusika haswa ni nani... Serikali za mitaa au serikali kuu.
   
 12. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SASA HIVI ITAUNDWA TUME YA MADIWANI ,IKIONGOZWA NA MEYA HUSIKA,.ITAFANYA UTAFITI ILI KUJUA NI SHERIA GANI INATUMIKA KUWEZA KUBADILISHA HAYO MAJINA,..HALAFU ITAUNDWA tume NYINGINE YA KUFUATILIA SABABU YA KUBADILISHWA HAYO MAJINA,..HII ITAONGOZWA NA KAIMU MEYA ,.IKISHIRKISHA MADIWANI WA SEHEMU HUSIKA NA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI,. BAADAYE ITAUNDWA NYINGINE YA KUBAINI NI KINA NANI WALIOFANYA HIVYO,.HII ITAONGOZWA NA MEYA, VIONGOZI WA DINI [MASHEHE,VIONGOZI WA MABOHORA,WAISHIO HUKO] WAKISHIRIKIANA NA POLISI
  ,..RIPOTI KAMILI IKIPATIKANA WAHUSIKA WATAPELEKWA POLISI,.
  NAO POLISI WATAANZA UPELELEZI KUMBAINI MUHUSIKA....
  BAADAYE WAZIRI HUSIKA ATAINGILIA KATI NA KUAMURU MAJINA YA ZAMANI YARUDISHWE...
  MANISPAA HUSIKA ITASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI SABABU HILO HALIPO KWENYE FUNGU LA BAJETI YA MWAKA HUU LABDA WASUBIRI BAJETI IJAYO,,..
  MADIWANI WA SEHEMU HUSIKA WATAIOMBA POLISI IWASAIDIE KUWABANA WAHUSIKA ILI WACHORE VIBAO VIPYA,..POLISI ITAKATAA NA KUSEMA SUALA HILO LISUBIRI MAAMUZI YA MAHAKAMA.,.
  HUKUMU YA KESI NAYO ITATOLEWA BAADA YA MIAKA MIWILI,..NAWASHTAKIWA WATARUHUSIWA KUJIDHAMINI,...
  MPAKA HUKUMU IJE KUTOKA BAADA YA MIAKA MIWILI,.WATU WATAKUWA WAMESHAZOEA MAJINA MAPYA YA HIYO MITAA,.HIVYO YAKIBADILISHWA WAGENI NA WENYEJI WATAPOTEA TENA
  ,...........WAKATI MWINGINE SYSTEM YETU YA KUFANYA KAZI BONGO INANIKUMBUSHA ,HADITHI KARUMEKENGE ALIVYOKATAA KWENDA SHULE.,....hawa madiwani na meya sijui kazi yao ni nini hasa...tabu kweli kweli
   
Loading...