Maporomoko ya udongo yaua Ulaya

Maporomoko ya udongo yaua Ulaya

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,308
141117052707_landslide_italy_switzerland_lugano_304x171_epa_nocredit.jpg


Watu wapatao wanne wamekufa kufuatia maporomoko ya ardhi kusini mwa Uswisi na kaskazini mwa Italia kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Wanawake wawili wamekufa wakati tope zito lilipovunja nyumba karibu na mji wa Lugano nchini Uswisi.

Katika mpaka, mstaafu na mjukuu wake wa kike waliuawa wakati maporomoko ya udongo yalipoifukia nyumba yao.

Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea katika eneo hilo, na nchi zote mbili zimetoa ilani ya tahadhari.

Viwango vya maji katika maziwa Lugano na Maggiore, ambavyo vilionekana kuwa chini ,sasa viko juu kabisa na kutishia usalama.

Maporomoko ya ardhi Italia

Makazi na maeneo ya biashara, kama vile shamba karibu na ziwa Maggiore nchini Italia, yamekatwa mawasiliano kutokana na mafuriko.

Eneo hilo limepata mvua zaidi katika siku chache kuliko ilivyotarajiwa kawaida katika mwaka.
Kingo za mto Ticino zimevunjika karibu na Vigevano kaskazini mwa Italia.

Kaskazini zaidi, katika mkoa wa Ticino nchini Uswisi, wafanyakazi wa uokoaji walikuwa wakiwatafuta watu walionusurika Jumapili baada ya matope kuporomoa kilima na kuharibu jengo.

Serikali ya Uswisi imesema wanawake wawili wenye umri wa miaka 34 na 38 walipoteza maisha wakati maporomoko ya udongo yalipokumba jengo moja katika kijiji cha Davesco-Soragno.

131205082857_italy_landslide_304x171_reuters_nocredit.jpg

Chanzo: BBC Swahili
 
Duuu... pole yao, kumbe hii makitu hadi wao inawagonga?
mie nilidhani ni UGANDA NA Equatorial Guinea pekeee.
 
Back
Top Bottom