Mapishi ya mboga mchanganyiko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mapishi ya mboga mchanganyiko
Pale unapokuwa na haraka ya kuandaa chakula kwa muda mfupi au umetoka kwenye mihangaiko na umechoka sana ni vizuri kuandaa chakula rahisi na ukafurahia na familia.


Mahitaji

1. Viazi ulaya 4 vya wastani
2. Hoho jekundu 1/2
3. Hoho la njano 1/2
4. Hoho la kiajani 1/2
5. Njegere 1 kikombe cha chai
6. Carrot 1 kubwa
7. Broccoli kidogo
8. Cauliflower kidogo
9. Kitunguu 1
10. Nyanya 1/2 kopo
11. Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula
12. Curry power 1 kijiko cha chakula
13. Coriander powder 1 kijiko cha chai
14. Tarmaric 1/2 kijiko cha chai
15. Olive oil
16. Chumvi
17. 1/4 ya limao

Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini yaani isiyounguza chakula kwa haraka kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha weka kitunguu swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi

Vikishakuwa tayari weka nyanya na chumvi.
Pika mpaka nyanya ziive kisha weka vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao,

Baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
 
Halafu hiyo mboga inaonekana ni kidogo kwa tarmaric, coriander na curry powder kwa kiwango hivyo.
 
Nilijua Kwa mabachela itakuwa nafuu kumbe mzunguko wote huo da labuda weekend nimetulia la sivyo hapana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom