Mapishi ya makange ya kuku

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,264
Points
2,000

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,264 2,000
Mahitaji
-Kuku 1
-Karoti 3
-Vitunguu 2
-Vinega
-Pilipili kiasi
-Mafuta ya kukaanga

Jinsi ya Kuandaa

-Kata kata kuku
-Kaanga kuku
-Weka vinega kwenye bakuli katia humo na pili pili
-Weka kuku funika bakuli tikisa ichanganyike.
-Chukua kikaango katia kitunguu na mwagia wale kuku
-Katia karoti acha zichanganyike kwa dakika 5
-Ipua na pakua

*Msosi huu wanoga kwa ndizi za kukaanga au kuchoma chips na hata kwa ugali.
*Si kuku pekee lakhasha pia waweza kutengeneza makange ya nyama ya mbuzi au ng’ombe pia.

========

LEO tutaona jinsi ya kupika makange ya nyama ya kuku ikiwa ni kutokana na mfululizo wa kujifunza kupika vyakula vya aina mbalimbali.

MATAYARISHO NA KUPIKA

Kuku 1

Mafuta ya kupikia lita 1

Tangawizi iliyotwangwa (kusagwa) vijiko vikubwa 3

Kitunguu saumu kilichotwangwa- kijiko kikubwa 1

Kitunguu maji kikubwa 1

Karoti kubwa 1

Pilipili Hoho kubwa 1

Ndimu 2

Chumvi vijiko vikubwa 3

Masala ya kuku (chicken masala) vijiko vikubwa 3

Nyanya ya pakti kijiko kikubwa 1

Nyanya kubwa 1

Pilipili 1

MATAYARISHO

Osha kuku wako vizuri kisha mkate vipande upendavyo.

Muwekee viungo vyako kama tangawizi, vitunguu saumu, ndimu 1 na kipande (kipande kimoja weka pembeni), chumvi vijiko 2, masala ya kuku vijiko 2 kisha mchanganye vizuri na muweke kwenye friji kwa saa mbili.

Kata karoti, pilipili hoho na kitunguu maji kwa urefu au umbo upendalo, ila viwe vipande vikubwa vinavyoonekana baada ya kuiva.

Saga nyanya iweke kwenye kibakuli.

JINSI YA KUPIKA

Chukua kikaango, mimina mafuta na yaache yapate moto wa wastani. Anza kumkaanga kuku taratibu mpaka aive. Tumia kikaango hichohicho, punguza mafuta yabakize kidogo kwa ajili ya kukaanga viungo vilivyobakia. Anza kukaanga kitunguu kisha weka pilipili hoho halafu malizia na karoti. Usikaange kwa muda mrefu kwani havitakiwi kuiva sana.

Weka nyanya ulizosaga, koroga na malizia kwa kuweka chumvi, masala, nyanya ya paketi, pilipili na ile ndimu kipande kilichobakia. Mimina kuku wako na mkoroge kidogo ili aenee vile viungo, kisha mtoe weka kwenye sahani. Hapo makange yako yatakuwa tayari kwa kula, unaweza kula kwa wali au ugali.
 
Liwagu

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2017
Messages
1,763
Points
2,000

Liwagu

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2017
1,763 2,000
Mahitaji
-Kuku 1
-Karoti 3
-Vitunguu 2
-Vinega
-Pilipili kiasi
-Mafuta ya kukaanga

Jinsi ya Kuandaa

-Kata kata kuku
-Kaanga kuku
-Weka vinega kwenye bakuli katia humo na pili pili
-Weka kuku funika bakuli tikisa ichanganyike.
-Chukua kikaango katia kitunguu na mwagia wale kuku
-Katia karoti acha zichanganyike kwa dakika 5
-Ipua na pakua

*Msosi huu wanoga kwa ndizi za kukaanga au kuchoma chips na hata kwa ugali.
*Si kuku pekee lakhasha pia waweza kutengeneza makange ya nyama ya mbuzi au ng’ombe pia.
Ngoja nimuonyeshe mkewangu, sijuiataweza!!.
 
Black Coffee

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Messages
1,736
Points
2,000

Black Coffee

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2016
1,736 2,000
Me pia mpenzi sana wa makange ngoja ni share kaujuzi kidogo
Mahitahi
Kuku -1
Limao -1
Hoho -1
Karoti-1
Kitunguu maji-1
Saumu kidogo kama punje -4
Aromat
Black pepper
Na Unga wa broccoli
Maandalizi
Katakata kuku wako size utakayo weka chumvi na limao na maji kidogo Chemsha kuku wako (me napenda wa kienyeji) nachemsha ili alainike ,kama niwa kisasa haina ulazima . Then ipua
Andaa pan yako weka mafuta mkaushe akauke vizuri then ipua
Andaa pan Safi weka mafuta kidogo weka Kitunguu kaangaa kidogo weka saumu thenKaroti na hoho kaangaa kigodo weka kuku wako changanya tia Aromat, black pepper,limao lilo baki koroga Wacha kidogoo lastly weka Unga wa broccoli Wacha kidogo then msosi utakuwa tayari kuliwa unaweza serve na chips, ndizi na Ugali
NB: viungo vyote Kata mfumo wa juliani Yaani kwa urefu
Pia spice ni kwaajili ya ladha tuu unaweza punguza au ongeza
 
Millie Mhb

Senior Member
Joined
Jun 29, 2016
Messages
189
Points
250

Millie Mhb

Senior Member
Joined Jun 29, 2016
189 250
Me pia mpenzi sana wa makange ngoja ni share kaujuzi kidogo
Mahitahi
Kuku -1
Limao -1
Hoho -1
Karoti-1
Kitunguu maji-1
Saumu kidogo kama punje -4
Aromat
Black pepper
Na Unga wa broccoli
Maandalizi
Katakata kuku wako size utakayo weka chumvi na limao na maji kidogo Chemsha kuku wako (me napenda wa kienyeji) nachemsha ili alainike ,kama niwa kisasa haina ulazima . Then ipua
Andaa pan yako weka mafuta mkaushe akauke vizuri then ipua
Andaa pan Safi weka mafuta kidogo weka Kitunguu kaangaa kidogo weka saumu thenKaroti na hoho kaangaa kigodo weka kuku wako changanya tia Aromat, black pepper,limao lilo baki koroga Wacha kidogoo lastly weka Unga wa broccoli Wacha kidogo then msosi utakuwa tayari kuliwa unaweza serve na chips, ndizi na Ugali
NB: viungo vyote Kata mfumo wa juliani Yaani kwa urefu
Pia spice ni kwaajili ya ladha tuu unaweza punguza au ongeza
Yanatofaut gan na nyama ya mchuzi
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2019
Messages
650
Points
500

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2019
650 500
Halafu Makange what is this word for?
hapo umepika/ kaanga nyama ya kuku. siyo sijui makange yenu hayo! usiharibu Lugha bana.

ukiongea kipare kuleee jukwaa la kipare, kaonane na kimambi
 
Forum statistics

Threads 1,344,277
Members 515,388
Posts 32,813,916
Top