Mapishi ya maharagwe na pilipili manga

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
Mapishi ya maharagwe na pilipili manga

Mahitaji
234204770.jpg


Maharagwe gramu 250, karanga gramu 100, karoti moja, koliflawa gramu 200, pilipili manga gramu 50,mchuzi wa sosi kijiko kimoja, siki vijiko viwili, sukari vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja

Njia

1. kata maharagwe yawe vipande, kata karoti iwe vipande vipande, na kata koliflawa iwe vipande. Kila weka kwenye maji joto, halafu vipakue. Weka karanga kwenye maji moto ichemsha kwa dakika 15, ipakue. Weka vipande vya maharagwe, karanga, koliflawa na karoti kwenye bakuli moja.
2. tia mafuta kwenye sufuria, tia pilipili manga, halafu tia mchuzi wa sosi, siki, sukari na chumvi korogakoroga, ondoa pilipili manga, mimina mafuta hayo kwenye bakuli, korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo ni tayari kuliwa.


Mapishi ya kamba-mwakaje na uyoga

Mahitaji
caoguxiaoren.jpg

Kamba-mwakaje gramu 400, mafuta gramu 30, uyoga gramu 70, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, ute wa yai, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, pilipili hoho moja, wanga vijiko viwili, chembachembe za kukoleza ladha nusu ya kijiko.
Njia
1. osha kamba-mwakaje, koroga pamoja na ute wa yai, mvinyo wa kupikia, chumvi na wanga. Kata pilipili hoho iwe vipande. Kata uyoga uwe vipande.
2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia kamba-mwakaje kwenye sufuria korogakoroga, tia vipande vya uyoga, pilipili hoho, halafu tia chumvi, sukari, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, mimina maji ya wanga, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa


Mapishi ya nyama ya kuku na pilipili manga

20070814_0fdec5a1c109ed880ef8kVbsfOj2cWd6.jpg
Mahitaji

Nyama ya kuku gramu 200, pilipili hoho gramu 50, pilipili manga gramu 20, pilipili mboga gramu 20, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, sukari kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, na mchuzi wa sosi vijiko viwili.
Njia
1. kata nyama ya kuku iwe vipandevipande. Kata pilipili mboga iwe vipande.
2. washa moto , tia mafuta kwenye sufuria punguza moto kidogo, tia pilipili hoho na pilipili manga kwenye sufuria, korogakoroga. Tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, korogakoroga, tia vipande vya nyama ya kuku korogakoroga, mimina mchuzi wa sosi, korogakoroga, tia vipande vya pilipili mboga, sukari na chumvi, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo kiko tayari kuliwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom