Mapishi ya Kuchoma na Kukaanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapishi ya Kuchoma na Kukaanga

Discussion in 'JF Chef' started by MziziMkavu, Dec 7, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,619
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mapishi ya firigisi za kuku
  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji[​IMG]
  Firigisi za kuku gramu 200, pilipili mboga moja, tangawizi gramu 5, pilipili manga gramu 2, vitunguu saumu gramu 5, mchuzi wa chaza gramu 5
  Njia
  1. chemsha maji, halafu weka firigisi ya kuku kwenye maji ya moto, halafu zipakue, na uziweke kwenye maji ya baridi. Kata firigiri ya kuku iwe vipande.
  2. kata tangawizi, vitunguu saumu, pilipili mboga iwe vipande.
  3. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu na pilipili manga kwenye sufuria, korogakoroga, tia firigisi za kuku kwenye sufuria, pilipili mboga, korogakoroga, mimina mchuzi wa chaza, korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Mapishi ya kamba-mwakaje na vitunguu saumu
  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji[​IMG]
  Kamba-mwakaje gramu 500, limao moja, vitunguu saumu gramu 10, vitunguu maji gramu 5, mchuzi wa sosi vijiko viwili, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, wanga wa pilipili manga kijiko kimoja
  Njia
  1. osha kamba-mwakaje, ondoa vichwa vyake.
  2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu saumu na vitunguu maji, korogakoroga, mimina juisi ya limau, mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, korogakoroga, tia wanga wa pilipili manga, sukari, mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga, mimina maji yasiyo ya baridi, korogakoroga halafu weka kwenye kamba-mwakaje.
  3. chemsha maji kwenye sufuria, weka kamba-mwakaje kwenye sufuria, chemsha kwa mvuke kwa dakika 10. mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.


  Mapishi ya samaki na mafuta
  [HR][/HR]
  [TABLE="width: 90%, align: center"]
  [TR]
  [TD="class: FontStyle5"]Mahitaji[​IMG]
  Samaki mmoja, mafuta gramu 50, supu ya kuku gramu 300, pilipili manga gramu 3, mvinyo wa kupikia gramu 20, mchuzi wa sosi gramu 30, chumvi gramu 4, chengachenga za kukoleza ladha gramu 3, giligilani gramu 30, vipande vya vitunguu maji gramu 20, tangawizi gramu 20
  Njia
  1. ondoa vitu vilivyo ndani ya tumbo la samaki, osha samaki halafu kata kata kwa kisu kwenye pande mbili za samaki.
  2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi, korogakoroga, halafu mimina supu ya kuku, mvinyo wa kupikia, tia chumvi korogakoroga, weka samaki kwenye sufuria, chemsha kwa dakika 15, halafu ipakue. Weka samaki kwenye sahani, weka vitunguu maji, tangawizi na pilipili manga.
  3. washa moto tena, mimina mchuzi wa sosi kwenye sufuria, mimina mafuta halafu mimina juu ya samaki, tia chengachenga za kukoleza ladha. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...