Mapinduzi yanakuja - bomu la ajira kwa vijana

Mapinduzi yanakuja - bomu la ajira kwa vijana

nyiondo

Senior Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
149
Reaction score
24
Mtumishi wa Mungu akisema werevu husikia na kuzingatia.
Nabii TB Joshua wa SCOAN amepewa ufunuo kuhusu MAPINDUZI ambayo yatatokea kama suala la ajira kwa vijana halitatekelezwa sasa. Hili litaanza kama maandamano ya vijana kukosa ajira - vijana wenye sifa zote ie wasomi na wengineo ambapo wataingia mitaani. Maandamano yatazimwa kwa nguvu na kadharika kama 'kawa' lakini mapinduzi hayazuiliki.

Ameoneshwa mapinduzi haya yataundwa kwa asilia 90 ya vijana kwa hiyo nini kifanyike>?
1. Ajira kwa vijana zitengenezwe hima ili kukabiliana na dalili zote za kuyazima mapinduzi
2. Vijana waingizwe katika 'uongozi' kwa maana kuwa, kama mwenyekiti wa chama ni mzee, msaidizi au makamu wake awe ni kijana na hili lifanyike kila seka
3. Wazee waliostaafu waondoke kwenye ofisi zao na kuacha vijana wafanye kazi

Kwa kuzingatia hayo jamii yetu itakabiliana na hizo dalili zote za mapinduzi na kuyazima. Kila nafasi ya uongozi ikiwa na msaidizi ambaye ni kijana itawezesha vijana kuanza kuivaa 'mikoba' ya wazee ili wanapostaafu mambo yanaendelea.

Wale wenzetu wa 'system' fikisheni ujumbe huu kwa mamlaka zinazohusika. Viongozi wetu wa nchi wafahamishwe kuhusu bomu hili litakalolipuka kama lisipozimwa kwa namna ambayo mtumishi wa Mungu amesema.

Mungu ibariki nchi yangu Tanzania ili haya yasitokee.
 
Nimemskia na anauambia ulimwengu mzima kazi kwa watawala wetu mwenye sikio na asikie Roho ayaambiavyo mataifa!
 
yaa...amesema hivyo,na km viongozi mna akili yafanyieni kazi haya,amesema mapinduzi makubwa yanakuja kutokea(yataletwa na vijana), stay tuned!!
 
yameshaanza arusha. msingoje utabili sababu dalili zimeshaanza
 
Back
Top Bottom