Mapinduzi yakifeli kinachofuata ni nini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
Huku kwetu mitaani wafanya vurugu waliandika ujumbe wao kwenye kuta na mawe maneno 'Samia must go'. Ndiyo nikajua ahaaaaaa kumbe hizi vurugu ndiyo namna yenyewe ya kupindua. Nilipoona maandaishi yale nikajua kuwa lazima watakufa watu wengi kama madhumuni ndiyo hayo. Lakini naona serikali bado imesimama hadi leo hii ipo.

Ni nini kitafuatia kwa serikali na wanamapinduzi baada ya mapinduzi kushindwa. Tutarajie kuona nini??
 
Serikali ya Mapinduzi Iko Zanzibar. Waulize walipofeli mara ya kwanza walifanya nini mpaka mwaka 1964 wakafanikiwa.

Upo chama cha Mapinduzi halafu unayahofu/kebehi Mapinduzi?
 
Samia Must go maana yake huyo sio Chaguo la watanzania, ameingia ikulu kwa mtutu wa Bunduki. Hana tofauti na magaidi wengine.
 
Kuviziana
Kwanza kulikuwa hakuna Mapinduzi wala jaribio la Mapinduzi. Mapinduzi hutanguliwa na njama... Tarehe 29/10/2025 hakukuwa na njama bali kutokuridhika kwa watanzania wengi wenye akili timamu kuhusu mambo mbali mbali.

Kuandika kwenye ukuta "Samia must go" bila ya vielelezo vya kimkakati ni maneno tu na wala si njama!
 
BAADA YA MAPINDUZI KUFELI NI MARIDHIANO MATAKATIFU . ILA SERIKALI HAINA KUNEGOTIATE NA WAHAINI .
 
Kila mharibifu atafikiwa kwa wakati wake.
Kama huna shida tulia kwa amani hakuna wa kukubughuzi ila kama una tone la mauzauza utafikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…