MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,591
Katika vitu ambavyo nikiwahi kuona haja ya kuvifahamu ni hii kitu ya majirani zetu na ndugu zetu.
Ninaamini kuna watu humu Wenda walikuwepo au wanauelewa mkubwa zaidi kuhusu mapinduzi haya ya kipekee na yenye kila aina ya mvuto na mambo yasiyona majibu.
Katika kufukuafukua huku na kule nimekutana na haya katika vyanzo vya kimagharibi kuhusu mapinduzi ya zanzibar.
1: Haya kuwa ya kutafuta uhuru maana uingereza walikuwa wameshawapa wazanzibar uhuru tangu 1963
3:kipindi hicho zanzibar ilikuwa na waafrika 230000 miongoni mwa hao walikuwepo waliojiita washirazi wenye asili ya Irani. Waarabu wachache kama 50000 na waasia Wa kusini kama 20000 ambayo weñgi wao walikuwa wafanya biashara.
4:Kwa mujibu Wa wanahistoria Sultan Jamshid alipata support na chama Chao cha ZNP na baadhi ya weusi kutokana na ukweli kuwa origin yake ilikuwa ni mchanganyiko tofauti na waarabu wengine pia walikuwa na pesa sana na walimiliki mashamba na ardhi kubwa. Ndio maana uchaguzi baadae walishinda japo waafrika mchanganyiko na washirazi ASP walilamika wamechakachuliwa na kufikilia kumpindua.
5:Mwaka 1961 katika kuwaandaa wawe huru waingereza walitunga katiba na kuitisha uchaguzi kati ya vyama hivi hasimu ZNP na ASP wakatoka droo kila mmoja kuibuka na viti11 ya wawakilishi. Na baadae kila uchaguzi ulipoitishwa viti viliongezeka na ZNP chini ya Jamshid walichukua vitu zaidi japo jumla ya kura waafrika waliongoza kitu kilichowafanya waamini wanahujumiwa na kupanga mapinduzi.
6:chama cha waarabu kwa kushirikiana na wapemba zppp ndio waliokabidhiwa uhuru na waingereza baada ya kuwagaragaza ASP katika uchaguzi Wa kidemocrasia. Lkn walipoomba ulinzi kutoka kwa waingereza wakakataa na hivyo kuwa na wepesi Wa kushambuliwa na weusi na washirazi maana walikuwa weñgi. Waingereza na intelijensia yao waliyaona machafuko na mapinduzi na kuona kutoa ulinzi kwa waliokuwa wanatawala ni kama kuongeza tatizo.
MAPINDUZI
Saa Tisa za usiku, Jan 12 1964 kati ya wapambanaji Wa kiafrika kati ya 600 hadi 800 walivamia kituo cha polisi na kuiba siraha naredio kisha kuanza mapambano na waarabu wachache na watu walipokuwa wanawaunga mkono.hadi kufikia mchana saa nane zanzibar yote ilikuwa imeshatekwa na sultani pamoja na waziri mkuu wake Mohammed Shamte Mohammad walikimbilia kwenye jahazi na kutokomea.
Inasemekana mapinduzi yalipangwa na karume mwenyewe japo siku hiyo yeye hakuwa zanzibar alikuwa bara huku, maana yeye na mwenzake Babu na chama Chao cha umma kilichoshirikiana na ASP kilikuwa kimepigwa marufuku na baadhi ya Askari waliowaunga mkono kutimuliwa. Walishauriwa na mganda Okello kukimbilia huko ambaye aliingia kisiwani hapo kutokea Kenya
1959 huko alifurushwa kutokana na kuhusishwa na kuandaa Maumau. Huyu aliwahi kuwa polisi Uganda na hadi wakati huo alikuwa katibu Wa ASP tawi LA Pemba. Na inasemekana anahusika kwa nafasi kubwa sana kuandaa mapinduzi
Sultani na wadau wake wakidhani kwa sababu wanashinda kihalali na kidemocrasia, waliomba msaada Wa kijeshi na kipolisi kutoka Tanganyika na Kenya zilizokuwa huru lakini hawakupata msaada wowote.
BAADAE;
1: umma na ASP wanachukua madaraka karume akaja kuwa rais
. Mission ya kwanza ni kukifuta na kukitupilia mbali chama cha kisultani ZNP na cha kipemba mshirika wake ZPPP.
2: kwa kumuhofia okello, alimtenga na siasa japo alibaki na cheo chake cha field marshal japo okello mwenyewe hakuwahi kwenda jeshini au kuwa mwanajeshi zaidi ya kuwa polisi Uganda.
3kello na wanamapinduzi wachache wanaitisha kisasi dhidi ya Waarabu na waasia kisiwani unguja, hii ilijumuisha kuwapiga,kuwabaka,kulazimiswa kuolewa,kunyang'anywa Mali na kuwavamia kila wakati.
4: haijulikani ni wangapi waliuwawa Bali okello mwenyewe alijinasibu kupitia media kuwa aliua maelfu, wengine wanasema 20000, vyombo vya kimagharibi wanasema kati ya 2000 hadi 4000.kampuni LA kiitaliano LA kutengeneza movie lilikuwepo zanzibar kwa herikopta lilipiga picha ya kaburi LA watu weñgi waliokufa kabla ya kufukiwa. Ikumbukwe kwa amri ya okello hakuna Mzungu aliyeguswa, Waarabu weñgi walikimbia na kurudi kwao Oman. Na wala mauwaji haya hayakufanyika Pemba kwa kiasi kikubwa.
5:Okello akatengeneza kikosi cha kijeshi Freedom Military Force kwa kushirikiana na wadau wachache wanamapinduzi wakawa wanarandaranda mitaani na kuvamia Waarabu na kuwaibia madukani. Kitendo hiki kiliwakwaza baadi ha wanaASP wenye msimamo Wa wastani maana kwanza jamaa ni mganda, pili ni mkristo alafu mbabe. Karume na kikosi chake wakawanyang'anya silaa FMF, siku okello akiwa anatokea huku bara alizuiwa na akipigwa marufuku kukanyaga ardhi ya zanzibar, akarudiswa Kenya na baadae kwao Uganda.hadi siku chache kabla ya muungano mwezi Wa nne FMF waliobakia wote walikuwa wamenyang'anywa silaha na karume kuamua kuungana na bara inasemekana moja ya sababu ni kupunguza nguvu member Wa Umma na ASP walipokuwa na msimamo mkali saana.
JE WAZUNGU WANGEWEZA KUZZUIA??
1: jeshi LA uingereza lililoko Kenya lilipewa taarifa taarifa saa kumina moja kasoro za asubuhi na sultani na wakawa standby dkk kumi na tano baadae kwa kuhofia damu kumwagika zaidi wakaongeza muda na kwa makubaliano na karume walipewa muda Wa kuondoka raia wake tu.
2:Masaa kadhaa manowali LA kimarekani liliwasili kuchukua raia wake. Kwa kosa LA kutokuomba kibali kwa wanamapinduzi lilishikiliwa chini ya ulinzi zaidi ya siku mbili na wababe hawa wakizanzibari kitendo kilichowakwaza sana wazungu Ila baadae waliachiwa. Ikumbukwe wamarekani walikuwa na kituo Chao cha kiuangalizi cha NASA zanzibar kipindi hicho.
3:inasemekana na wamagharibi mapinduzi yalipewa support na wacommunist ikiwepo Cuba,Russia. Na msaada Wa watanganyika hii ni kutokana na ukaribu Wa Osca Kambona na wakina babu katika sakata hili. Pia memba weñgi Wa Umma na wapambanaji wao walionekana wakiwa na style ya mwanajeshi Wa Cuba hasa kufuga ndevu mfano Wa Fidel Castro na ishara nyingine nyingi. Kuwepo kwa washauri wengi waliokuja baada ya mapinduzi kutokea CHINa, USSR na UJERUMaNI mashariki. Pia zanzibar ikawa nchi ya kwanza afrika kuitambua Jamuhuri ya kidrmocrasia ya ujerumani na nchi ya KOREA KASKZINI.Mwanamapinduzi Sugu aliyepanga mapinduzi sehemu nyingi duniani CHE GUAVARA alisikika akijinasibu kuwa zanzibar ni mshirika wetu wa karibu lakini alikana uwepo wa vikosi vya CUBA katika mapinduzi hayo.Pia gazeti LA kimarekani NEW YORK TIMES likiandika kwa taadhari kuwa Zanzibar inaeleke kuwa CUBA ya AFRIKA.
4:Kuwepo kwa Jasusi na Mmossad lililokubuhu LA Kiisrael katika ardhi ya zanzibar siku ya mapinduzi. Jamaa huyu David KIMCHE. Jasusi hili linasadikiwa kuwa na mkono wake katika mapinduzi hayo.
5: wakati haya yakiendelea waingereza na kikosi vyao walikuwa makini wakifuatilia kila atua zanzibar hasahasa Okello na kikosi chake asijeakawazidi nguvu ASP walipokuwa na msimamo Wa wastani na kuitawala zanzibar kibabe. Askari Wa mwamvuli, memeli ya kivita yaliyokuwa na herikopta na jeshi LA wanamaji walikuwa standby kama hayo yangetokea na jamaa kuanza kunyanyasa wazungu.
6: muunganiko na Tanganyika ulitia wasiwasi Wenda wanaumma wakaanzisha mapinduzi mapya kwa kutokukubali makubaliano ya karume na nyerere. Waingereza waliandaa Makomando wao na operation Kabambe iliyoitwa OPERATION SHED. Hii ni herikopta zikizobeba magari maalumu yatakoingia unguja na kumlinda karume na serikali yake endapo wenzake wangepanga kumpindua. Hii haikufanyika maana kilichotazamiwa hakikutokea.PLAN GILALDA iliandaliwa pia na uingereza, kikosi maalumu kutokea baharini kumlinda na kumsaidia NYERERE endapo UMMA wangeamua kuvamia dar es salaam na kumuangusha Mwalimu.
Hadi kufikia December mwaka 64 operation zote zikafutwa na huo ndio mwisho Wa muingeleza kuingilia kivita Tanzania.
MWISHO
Mapinduzi ya zanzibar yanabaki kuwa tukio LA kuvutia na LA aina yake katika ulimwengu Wa WASOMI,WANANZUONi na WANAHISTORIA na sisi HUMU jukwaani wapenzi Wa kutafakari na kuchambua kila kitu kwa mitazamo huru.
Kwa wazanzibar weñgi ni Hitimisho LA ukaliwaji Wa Waarabu na wenye pesa kwa waafrika masikini iliyodumu zaidi ya miaka 200. Japo wakati wanatolewa walikuwa wnatawala serikali ya shirikisho iliyoshinda kidemocrasia.
Kuzaliwa kwa chama pendwa na lalamikiwa cha CCM.
Karibu kwa tujadili,kukosoa, kurekebisha, kutoa unachojua, changamoto, au nyongeza maana Wenda zilikuwepo au au baba au babu yako alishiriki na kukipa hali halisi.
Vitu hivi sikuwahi kuvisiikia darasani. Elimu haina mwisho..
........