Mapinduzi ya simu za mkononi... Tuandike historia.

Ramos

JF-Expert Member
May 13, 2010
498
130
Kati ya evolutionary events zilizotokea katika zama hizi hi sim za mkononi. Kwenye miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000, umaarufu wa simu za mkononi ndio ulikuwa unakuja juu Tz. Kwa vijana wanaokua leo, itakuwa vizuri tukiwapa experience ya jinsi simu hizi zilivyoibukia na vituko vyake.

Binafsi, wakati naona sim ya mkononi kwa mara ya kwanza mwaka 1997, sikuamini kama kuna siku maishani mwangu ningekuja kumiliki kitu cha 'thamani' kama kile. Nilikuja kusoma stori ta Abdalah 'King' Kibadeni alipokuwa amemshtaki 'changu doa' kwa kumuibia simu, nikazidi kuona kama simu kilikuwa kitu cha hali ya juu sana.

Wana Jf ambao mmeshuhudia kuingia hadi kuzagaa kwa technolojia hii, hebu mwageni hapa jinsi mnavyoweza kuyaelezea mapinduzi haya japo kwa kifupi...
 
Mmmmmh ilikuwa shughuli mwana, kwanza mtu mwenye simu alionekana kama mtu wa pekee sana, mtu mwenye vyake na anaweza kukunyanyapaa na ukashuka hivi hivi unajiona. Naikiita hiho simu ndo utacheka ukome mtu atakurupuka na kukimbilia upande mwingine. atakwenda na kurudi kwenda-kurudi huku anaongea mpaka mimi nilidhani huwezi kuongea Kwa simu ukiwa umekaa au kusimama - ni vituko!
 
nakumbuka miaka ile ya 1997 ndipo wazazi walinunua simu saresare zilikuwa siemens kidole juu,lol nilijiona nipo ktk familia ya kitajiri ,ukishika simu ya baba yani ni bonge la kipigo toka kwa mshua.,lakini leo simu ni kitu cha kawaida hadi watoto wa shule za msingi wanazimiliki
 
Kuna mama mmoja mwaka wa 1999 alinunuliwa simu na mumewe,siku ya pili akampigia kumbe simu ya jamaa ilikuwa haina chaji akapata jibu 'simu unayopiga haipatikani jaribu tena baadae' kwa sauti ya kike.Mama akafoka sana 'we mwanamke unaepokea simu ya mume wangu ni nani na kwanini uipokee wewe' ? Jioni ilikua kesi kubwa sana nyumbani pale mpaka mumewe akamwelewesha kwa kuizima na kumwambia aipige.
 
ha simu ilikuwa mpango mzima,nakumbuka ,Ulikuwa ukinunua unaletewa mpaka home,jamaa anakupa maelezo on how to do it,alafu pia unaenda kulipia pale ktk ofice za mobitel[now Tigo] kulikuwa na bonge la foleni ya kulipia kwa dola.

Duh!sasa kituko ilikuwa ktk Msiba,mtu akija kulala msibani na simu yake,full madoido,na inakuwa gumzo kwa wafiwaa na kusahau hata msiba wenyewe
 
hii topic imenikumbusha mbali. mimi nakumbuka kwa mara ya kwanza niliona mtu anashika simu mwaka 1998 nikiwa chuo kikuu. kwa bahati mtu huyu alikuwa room mate na course mate wangu. kwa kweli watu wote darasani tulikuwa tunamuona ni mtu wa matawi. hata yeye alikuwa anajiona yuko tofauti na sisi. kadri ya muda ulivyoenda ndipo tuliendele KUSHUHUDIA baadhi ya watu wachache darasani wakishika simu, tena wakati huo Siemens ilikuwa juu. Kwa Kweli, TUMETOKA MBALI
 
ha ha haaaaaaaaaa, mmenikumbusha mbali sana!!!!!

nakumbuka mara ya kwanza kuwa na simu nilikuwa najifungia kabatini nampigia jamaa yangu usiku!!

sitakaa nisahau duh!!
 
Kwanza mimi sikuamini kama unawezakupiga ktk landline
*Niliamini nikama radiocall
*Niliona kama nikitu cha ajabu sana
*Siku moja nikaenda mobitel kununua zililetwa za poromotion kubwa hizo baadae wakaleta nokia ringo ndo ilikwa ndogo ikaja sasa gsm nikaletewa simu kamanokia ringo kwenda tritel wakasema imelockiwa hivyo haiwezi kufanya kazi hapa dah nanilikuwa nimeinunua pesa nyingi laki2 zikaenda na maji!!
 
Jamani manaikumbuka trytell......ukipigiwa unachajiwa.....ukipiga unachajiwa....ilikuwa ni garama ya kufa Mtu...halafu ni Dola...ilipoingia voda kwa siku ya kwanza tuu zaidi ya Wateja elfu tatu wa trytell walihamia Voda....Ndio ukawa mwanzo wa kifo cha trytell......trytell ndio ulikuwa mtandao wa kwanza Digital!!!!!!
 
1. Inanikumbusha simu ya kwanza kuiona. Ilikuwa ni Mobitel aina hii

fig-7.jpg

2. Then zikaja motorola zile ambazo unaweza kuweka battery za kawaida (betri za redio) kama ukiishiwa charger.

3. Then zikaja Ericson nick named 'Mshindi'

4. Then ikaingia Nokia era..6600, 2100, 1100 , 3100, Motorola pia zilikuja Razr, 'Roundabout' he he he

5. Alafu akaingia NCKIa, Nokla , Pikachuu etc

6. Now watu wanataka Blackberry, Iphone , (HTC- Android phones) na lately Ipad

7.NEXT.. Smartphones ERA..

B.P (2011)
 
Back
Top Bottom