Kwanini CCM ikafuta na baadae ikarudisha uchaguzi Zanzibar?
CCM kumnyang'anya ushindi Maalim Seif katika uchaguzi wa Oktoba 2015 wamefanya mapinduzi ya pili Zanzibar. Wameondosha dimokrasia kwa mara ya pili na kuleta utawala wa mabavu. Haya mapinduzi ya sasa yanatufahamisha maana ya ule usemi wa CCM Zanzibar "Mapinduzi Daima". Alipo sema marehemu Asha Bakari: "Serikali hatuitoi kwa vikaratasi", hapana aliemrudi au kumkosoa kutika wakuu wa CCM. Alikua akikisemea chama chake. Demokrasia Tanzania inakufa.
Wasiwasi wa CCM kushindwa uchaguzi Zanzibar ulikuwamo kwenye vichwa vya kila mtu Tanzania. Masuala yanayofaa kujiuliza ni haya:
Kwanini CCM haikuchukua hatua za kuzuia CUF isishinde tokea mwanzo?
Kwanini CCM ijitie kwenye fedheha ya kuvunja matukio ya uchaguzi na kubidi kurejelea uvhaguzi mpya?
Kwahakika uongozi wa CCM walifanza makosa kumuamini Shein na wana-CCM visiwani kwamba wataweza kuyadhibiti mambo huko visiwani. Ukweli wa mambo viongozi wa CCM Zanzibar hawakua na uwezo wala ujuzi wa kudhibiti mambo ili CUF isishinde. Kiburi yao hao viongozi wa CCM kwa kua wananguvu za vyombo vya serikali zimewaleva wakasahau nguvu za raia wapigakura.
Kwanini CCM bara isiingilie mapema kuepukana na fedheha ilio fuatia baadae?
CCM bara, kwakuongozwa na Rais Kikwete ilijua vizuri kwamba CUF itashinda Zanzibar mambo yakienda kihalali. Lakini Rais J.M.K aliamini kwamba Rais Shein ataweza kuchezea na kubadilisha matukio ya uchaguzi.
Pia CCM ya bara ilimshughulikia sana Luwassa na UKAWA na wakawaachia wenzao visiwani wa mshughlikie Maalim Seif na CUF yake. Jamaa wa CCM Zanzibar hawakua na akili wala ujuzi wa kuweza kuzuia CUF isishinde. Matukeo ni hili fujo tulionalo.
Nini hali Zanzibar baada ya marejeo ya uchaguzi?
Baada ya Shein kupata 91.4% ya voti, CCM itaunda serikali pekee.
Kwa ukosefu wa dimokrasia, Wafadhili watakata misaada yao kuipa Zanzibar bali pia na Tanzania bara itakosa misaada ya nje.
Shida za maisha na ughali pamoja na kuanguka thamani ya pesa za Tanzania zitaendelea kwa nguvu kubwa.
Maovu yanayowakuta wafuasi wa CUF Zanzibar watayapata wafuasi wa UKAWA Tanzania bara. Kukamatwa na kuadhibiwa kwa mashekhe wa Zanzibar huko bara pamoja na kukamatwa nakupigwa muandishi wa habari Salma Said Dar es Salaam ni mifano ya maovu yanayo fanzika Tanzania bara. Leo yanawakuta Wazanzibari kesho watayaona Watanzania bara,
Upinzani utazidi kasi na shida za maisha na ukosefu wa dimokrasia zitapelekea fujo za ugaidi kuanza Tanzania.
Udini utashika kasi nchini kwa Watanzania kujua CCM imempindua Maalim Seif kwa kufuata maonyo ya kidini ya viongozi wa CCM bara kama Lukuvi na Sitta.
Kuhusu mambo visiwani Zanzibar kuna dalili kwamba tumerejea ya kale. Kugombana wenyewe kwa wenyewe na kumuona mtu wa mbali kua ni muokozi. Kama Nyerere hakuweza kua muokozi wa Zanzibar Januari na April 1964, hawezi Magufuli leo kua muokozi. Magufuli na wenziwe bara (Akina Kikwete, Lukuvi na Sitta) ndio wapika jungu, na leo ulimwengu unawabembeleza waiokoe Zanzibar. Unakumbuka Nyerere alivopika jungu la kuivamia Zanzibar na ulimwengu ukamuomba aimeze Zanzibar kabisa?
Wazee wanasema: “Ugomvi wa panzi ni faida ya kunguru”. Wazanzibari leo wamegawanyika tena baada ya kuungana kwa mara ya mwanzo waliposikilizana Rais Amani Karume na Maalim Seif Shariff mwaka 2010 kuunda serikali ya “Mwafaka”. Leo Rais Magufuli anapata nafasi nzuri kuingilia mambo Zanzibar kutekeleza ndoto ya Mwalimu Nyerere ya kuifanya Zanzibar jimbo la Tanzania na kuunda serikali moja tu.
Nini wafanye CUF?
Kwanza inabidi CUF waache kuzozana na mkia wa CCM ulioko Zanzibar. Hawa Rais Shein na Balozi Ali Seif iddi ni sawasawa na marhemu Asha Bakari na Borafia na Baraka Shamte. Hawana lao jambo. Wanafuata amri za CCM bara kutoka Dar na Dodoma. Kwanini CUF kupoteza wakati kupambana na mkia na kuacha kichwa?
Pili CUF itangamane kikweli na wenzao wa UKAWA. Upinzani wa Zanzibar na wa Tanzania bara una lengo moja. UKAWA imetambua mapema kwamba Linalo wafika wazanzibari litawafika wao pia. Usalama wa Taifa la Tanzania lipo kwenye dimokrasia tu. Waislamu, Wakristo, Wazanzibari na Watanganyika wa mjini na wa mashamba wanaume na wanawake wote watafaidika ikiwepo dimokrasia ya kweli na kila mtu akapata haki yake sawasawa.
Tatu ni kutumia vyombo vya dola kudai haki ilioporwa. Mpaka leo CUF haikushitakia mahakama za Zanzibar wala za Tanzania bara dhulma zilizopita. Baada ya kutumia vyombo vya sharia vya nchi na wakikosa haki yao wanaweza kutumia mahkama za Afrika ya Mashariki na za Afrika na za Ulimwengu.