Mapinduzi ya kidemokrasia kenya.

Mapinduzi ya kidemokrasia kenya.

Night Watch

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2017
Posts
2,102
Reaction score
2,152
Wasalaam wanajukwaa nadhani wote tu wazima na sikukuu ya eid imekuwa njema,ngoja niende kwenye mada. Nadhani ndugu zangu tumeweza kushuhudia leo maamuzi ya mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi nchini kenya,sisi kama watanzania kuna jambo muhimu la kujifunza katika maamuzi haya ya mahakama.Tumeshuhudia mahakama kenya kuwa na nguvu kubwa katika masuala ya nchi,lakini nguvu hii ya mahakama imekuja kutokana na wao kuwa na katiba iliyo bora. Hivyo watanzania hatuna budi kutafuta katiba mpya itakayo ipa nguvu mahakama zetu.Mfano mzuri kwenye uchaguzi wetu mwaka 2015,mmoja wawa wagombea alitaka kwenda kupinga matokeo kwenye mahakama za kimataifa,hili jambo ni kiashiria tosha kuwa mahakama zetu hazina nguvu.Tunahitaji katiba mpya na ndio ukombozi wetu vinginevyo tutaendelea kubaki hapa hapa tulipo sasa. Nawasilisha.
 
walikuwa wakali sana katika ile katiba pendekezwa kwa warioba

Sodhani kama hata kama tutapata kariba itakayokidhi wananchi wetu.
Na shida hiko hapo kwenye kupata katiba inayostahili.
 
Back
Top Bottom