Mapinduzi ya fikra bado yamefichwa katika kitabu ambacho bado haujafikiria kukisoma.

Babafetty

Senior Member
Nov 11, 2013
102
250
Nimefurahishwa sana nliposoma tweeter Account ya Zitto Kabwe, akieleza kuwa kwa mwaka huu amefanikiwa kusoma vitabu zaidi ya 50,
Huku akiwa ameshindwa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya mwaka 2013 alipoweza kusoma zaidi ya vitabu 60,
Ukweli ni kwamba hauwezi kubadilisha mtazamo wako na kuukomaza kwa kupiga soga na kubishana,
Waliofanikiwa zaidi ni wale walioweza kuchambua mawazo ya wenzao kupitia usomaji wa vitabu nje ya utaratibu wa vitabu vya darasan,
Kwan kupitia utamaduni wa vitabu ndiko unaweza kulisha ubongo wako iman na chakula cha mtazamo mpya...
Mara kadhaa tumekuwa tukiwakuta vibabu na vibibi vya kizungu wakijisomea vitabu ktk treni na mabas, na huko ndiko kunawafanya wawe wachambuzi wazur zaidi kuliko sisi tunaoishi Afrika,
Ningependa kuwashaauri vijana wenzangu kutafuta baadhi ya vitabu vya watunzi maridadi km Stephen Convey, Smith na wengneo weng kisha kujisomea ili kukomaza uwezo wa kutafakari na busara,

Kwan bila mapinduzi ya kifikra utakua mtumwa milele.
 

pistmshai

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,315
2,000
Habari yako mkuu...!

Nakuunga mikono yote miwili.. juu ya hili.
binafsi hata mimi mwenyewe nilipoanza kujenga hayo mazoea ya kujisomea vitabu tofauti na vya masomo ya darasani, niliona hata uwezo wa kutatua matatizo yangu binafsi umeongezeka.
Hata katika mazungumzo, niliona nimeanza kuwa imara katika kujenga hoja na kukubali mawazo/maoni ya wenzangu yale ambayo niliona yananijenga,niliacha tabia ya kupaza sauti, nilijifunza pia kubishana kwa hoja.

NAMSHUKURU SANA RAFIKI YANGU JONH KASANGA KWA KUNIFUNDISHA MENGI, MUNGU AMZIDISHIE MAISHA MAREFU.
 

kopites

JF-Expert Member
Jan 28, 2015
5,764
2,000
Mim kusoma vitabu kwangu ilikua kazi ngumu sanaaaaaaa,ila nashukuru mwaka huu wa 2016 nimesoma vitabu 3.nimejua vitu vingi nilivokua sijui na kuongeza kujiamini ktk mambo yangu
 

bavitamlewa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
271
250
Hongeren sana kukomboleka kifikra kupitia vitabu m pia ni mmja wenu ,,ni dhahiri umekomboleka naona una uwezo wa Ku recognize and appreciate especially kwa rafiki yko pistmshai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom