Acheni kujiona mastaa wakati hata uhakika wa uji tu hamna.Acheni kukopi hadithi za wenzenu,maisha na mikasa ya tz inatosha kuuza kwingine kwakuwa wanapata cha kujifunza toka kwenu.Mkiigiza vya kwao kipi kinakuwa kipya?Zingatieni elimu ya sanaa na fani zingine mbalimbali msibweteke na tulaki tuwili kujiona mnajua.Acheni kutengeneza "scandal"na magazeti nyie fanyeni kazi.Acheni kuingilia taaluma za sanaa kila mmoja abobee eneo lake kisanii.Kama ni muigizaji igiza kama ni muongozaji ongoza kama ni muandishi andika kama ni mhariri hariri kama ni mpiga picha piga picha acheni tabia ya kwenye movie mpaka mpishi ni huyohuyo mnaharibu watu hawawajibiki ipasavyo