Mapinduzi Sudan, Bashir kutoshtakiwa nje ya nchi

Mapinduzi Sudan, Bashir kutoshtakiwa nje ya nchi

Dav jm

Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
58
Reaction score
46
'Hatumsafirishi Bashir' "Bashir atashtakiwa katika mfumo wetu wa mahakama," Lt Jen Omar Zain al-Abidin amewaambia wandishi habari Hatutowavumilia wale wanaowaua raia," amesema.

Ameongeza kwamba hakuna raia wa Sudana atakayesafirishwa kwenda kujibu mashtaka katika nchi ya nje ilimradi baraza la jeshi lipo uongozini,lakini ameongeza huenda Serikali ijayo ya kiraia ikaamua kulishughulikia hilo kwa njia tofauti.

Bashir anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu katika mzozo wa Darfur magharibi mwa nchi hiyo.

Mzozo huo ulianza mnamo 2003 baada ya waasi kujihami kwa silaha wakiituhumu serikali kwa kuwanyanyasa watu wa kutoka eneo hilo. Maelfu ya watu waliuawa katika mzozo huo.

Lt Jen Awad Ibn Auf ameapishwa kama kiongozi wa baraza la jeshi Sudan linalotarajiwa kusimamia serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuingia katika serikali ya uongozi wa raia.
 
Hao viongozi wa kijeshi waliompindua Bashir wao pia wanatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita huko Darfur hivyo wao kumpeleka Bashir huko ICC ni Sawa na kujikata mkono labda uchaguzi ufanyike ije serikali mpya ya kirai ndio haki kwa raia wa Sudan itapatikana.
 
Natumai Bashiri hakuamrisha wafungwa wafanye kazi ngumu na kupigwa mateke.
 
Back
Top Bottom