Mapinduzi ndani ya CCM yanayumbisha nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapinduzi ndani ya CCM yanayumbisha nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ground Zero, Jan 6, 2012.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Mapinduzi ni chama ambacho katika uanzishwaji wake kilikuwa na malengo ya dhati ya ukombozi si tu kwa mtanzania lakini pia bara zima la Afrika. Ni vigumu kwa mtu mwenye akili timamu kupuuza mchango wa CCM katika kuunganisha Tanzania kama taifa.

  Mimi nilipata fursa ya kwenda kijijini katika mapumziko ya mwisho wa mwaka. Nafasi hiyo niliitumia kwa mapumziko lakini pia kwa kujifunza na kutafiti kuona mambo mbalimbali katika mtazamo wa watanzania wa kawaida. Katika kutafiti nilitaka kujua wananchi wanaonaje mfumo wa siasa wa sasa, walikuwa wanazungumza matatizo na mafanikio kwa kukihusiha na ccm na wangetamani mabadiliko kwa kuwa ccm ya sasa ina matatizo sugu ya rushwa.

  Kwa wale wanaokijua CCM wanakiri kuwa kilikuwa chama cha utu, kilichopambana na ubinafsi ndani na nje yake kwa manufaa ya wengi. Ni bahati mbaya, wengi niliokutana nao wanaoililia ccm ni wazee wengi wao wakielekeza lawama kwa vijana ambao wamepindua lengo la chama hicho cha kujenga jamii iliyosawa na kuanza kujenga matabaka kwa kujilimbikizia mali.

  Wengi wa watu wenye mapenzi na ccm wanadai kwamba ccm iliyoamini juu ya usawa wa binadamu na umoja wa waafrika wote hakipo madarakani, ilishapinduliwa na mtandao usiyoamini ama kuelewa vyema dhamira ya chama kile kilicho amini juu ya usawa wa binadamu kwa misingi ya utu. Kundi ambalo limeshika madaraka kwa kutumia jina la ccm ndicho kinachoyumbisha nchi, si tu kwa kushindwa kuwapatia watanzania unafuu wa maisha lakini hasa kuondoa hata matumaini madogo yaliyojengeka huko nyuma.

  Baadhi ya wale niliyozungumza nao walinieleza kwamba ili ccm ijirudi kwenye misingi yake lazima kipate nguvu ya ndani ya haja ya mabdiliko, na nguvu ya ndani hutokana na kujitafakari kwa kina. Lakini wakaonesha wasiwasi wao juu ya uwezekano wa tafakuri tunduizi ukiwa kwenye madaraka, kwa hiyo njia pekee ni kuondolewa madarakani ili upate muda wa kujitafakari na kujisafisha ili utakaporudi uwe na sura na mvuto halisi.

  Je ccm ina namna ya kujisafisha kikarudi kwenye misingi yake halisi kikiwa madarakani?Mapinduzi ndani ya ccm yakuwa ni vita ya kundi moja kupindua lingine kwa lengo la kushika madaraka.

  This was a private study, no scientific methods were applied, therefore it is more of an opinion than scientific .
   
Loading...