Mapigano ya makundi ya wahuni Marekani yaua 9

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,092
Reaction score
7,236
watu 9 wafariki baada ya mapigano makali ya kutumia silaha baina ya makundi ya kihuni zaidi ya 5 kupambana vikali huko Texas Marekani.

 
Yangetokea nchi ya Afrika mauaji ya aina hiyo Marekani ingeshalaani vikali na hata kuondoa raia wake na kufunga ubalozi wake.

Hilo nalo neno... sasa nae leo "nyoka kaingia nyumbani kwake".
 
Juzi nilikuwa naangalia nat geo documentary kuhusu hizi bike gangs na jinsi wanavyoishi afu jana nasikia wameuana aisee hawa watu ni noma
 
Ugonvi wao ulianzia kwenye parking, mmoja wa biker gangs alipaki sehemu ambayo ni kwa wapinzani wao. Uhuru wa maisha ya Marekani huwa hata siuelewagi.
 
haraka sana wakenya wakati ndio huu, toeni travel advisories kuhusu security ya united states kwa wakenya, mlipize kisasi walau kidogo MK254, hbuyosh
 
Last edited by a moderator:
Neno Bandidu la kibongo limetokana na hiyo gang The Bandidos.... Jamaa wana mkwaraaa eti 1% MC, yaani kuongea 1%, vitendo 99%.
Bandidos.

Asante.
 
Hayo majamaa yavokaa-kaa, kama hawajanyang'anyana mademu basi kulikuwa na ubishano kati ya kundi moja na jingine kuhusiana na ubora wa kitu au watu fulani au mitaa yao wanayoishi kiasi kilichopelekea mapigano hayo!!

Kwa sura zao tu hawa ni watu wasio na kazi zaidi ya kukaba watu, na kujivunia kwa mavazi,cheni, wanawake na vitu kama hivyo. Ukiibuka ubishani mdogo tu mauaji kama hayo ni vitu vya kawaida kwao. Tena waweza kuta hao ni moja ya wanajeshi waliopunguzwa kwenye Jeshi la Marekani hivi karibuni.

BACK TANGANYIKA
 
Ukiweza kujua idadi ya vifo vinavyotokana na kuuana Wamerakani wao kwa wao utachoka kabisa. Kifupi Marekani ni nchi ambayo usalama wa ndani ya nchi kwa raia wake ni mdogo sana. Jamaa wapo busy na kulinda mipaka na kufuatilia siasa za nchi za mbali.
 
haraka sana wakenya wakati ndio huu, toeni travel advisories kuhusu security ya united states kwa wakenya, mlipize kisasi walau kidogo MK254, hbuyosh

Ha ha ha,wenzio wamejazana ubalozini wakiomba viza ya kwenda Marekani,watakuelewa kweli na ushauri wako?
 
Last edited by a moderator:
yaap hata mimi,sasa mbona wankuaga wazungu tupu? kama lile la Hells Angel?

Kama umeangalia zile mugshots zao utajua kuwa hao waliokamatwa wote siyo wazungu.

Ila wazungu nadhani wapo wengi zaidi.

Sasa wewe umeziona hizo mugshots zote 170?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…