Mapepo ya kisiasa yanavyosumbua waandishi Tanzania

haki na usawa

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
481
135
Mapepo ya siasa ni mabaya sana! Waandishi sasa wameshakuwa watu wa kukaririshwa nini waandike na nini wasiandike! Waandishi sasa wameshakuwa na ugonjwa wa kufikri hata maswali madogo! Waandishi sasa wamepatwa na mapepo ambayo ni mabaya kupindukia! Waandishi wa sasa wahahoji kwanini na ilikuwaje?

Mbona umesema hivi mwenzio kasema hivi nawe wasemaje kwa hili? Waandishi sasa ni wagonjwa hakuna gazeti linaloleta tafakuri ya kiina juu ya migogoro ya vyama vya siasa mfano CHADEMA na CCM. Waandishi wa sasa wamekuwa wa kusikiliza upande mmoja na kuripoti bila kupata upande wa pili?

Na hata wakipata upande wa pili hakuna maswali ya msingi yanayoulizwa kuonyesha kuwa kweli waandishi wanafikiri? Waandishi sasa wameamua kuacha watu wachambue baya na zuri bila wao kutoa mwongozo wa hoja! Habari nyingi zinapotoshwa hakuna mwandishi anayechukua muda kufuatilia! Waandishi wa sasa ni wa kulipwa kama hulipwi huandiki taarifa zake vizuri!. Waandishi sasa wamegeuka wapiga debe wa wagombea viti mbalimbali!

Wandishi sasa wamekuwa ni watu wanaotaka kujineemesha kupitia kauli za kukizana mfano leo kasema kipo kesho kasema hakikuwepo muda mrefu! Waandhishi wa sasa ni kuandika tu bila kupanga hoja na bila kufikiri jana aliandika nini juu ya maada inayoendelea! Waandishi wa sasa wataka soft copy maana kufikiri kumepungua! maana mwandishi anapochapa atajua hoja ipi aweke na ipi asiweke!


Ushauri Chimbueni kiini cha tatizo na muache kuaminisha watu uongo maana vyombo vingi vya habari vinatoa taarifa ambayo iko mbali kabisa na ukweli uliopo huku ikiacha wananchi na maswali kibao yasiyo na majibu
 
Back
Top Bottom