Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 2,437
- 4,932
Je, kweli kuna mepepo, maruani na majini, au yote haya ni hadithi za imani na tamaduni? Katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo ya charismatic kama Walokole, watu huamini kwa nguvu kwamba roho au mepepo zinaweza kuingia mwilini wa binadamu, na hivyo kuonyesha ishara za ajabu kama kurukaruka au kutokwa na sauti.
Madhehebu mengine kama Katoliki au Wasabato wanatofautiana, wanatambua uwepo wa roho na malaika, lakini hawasisitizi matukio ya kimwili. Katika Uislamu, kuna imani kwa viumbe visivyoonekana vya kiroho, vyaani jinn, lakini kuingiliana kwa nguvu za kimwili si ya kawaida. Kwa upande mwingine, falsafa na sayansi zinaangalia matukio haya kwa mtazamo tofauti sayansi haijathibitisha kuwepo kwa nguvu hizi za kimwili, na mara nyingi inatoa tafsiri za saikoloji, hali za kiakili, au tamaduni za kijamii kama sababu ya matukio ya kurukaruka.
Mdau tuambie maoni yako kuhusu hili suala.