Mapenzi Yangu kwa Chadema!

Mapenzi Yangu kwa Chadema!

MTA1

Member
Joined
Jun 1, 2013
Posts
89
Reaction score
11
Waungwana nawasalimia kutoka mashamba ya chai, nipeni nafasi ya kunisikiliza; CHADEMA ni chama kinachonivutia kwa maneno mazuri ya Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe; kinadharia wana kila sababu ya kupewa nchi. Hatahivyo nimejiunga nacho ndipo nikakuta hali tofauti ndani ya chama wala hakina dhamira ya kuchukua nchi. Matendo ya viongozi waandamizi yanaashiria hawako tayari kuchukua dola 2015, badala yake wametanguliza matumbo yao mbele. Walipofika Lushoto mwaka 2010 kipindi cha kampeni nilijitolea kwa hali na mali kuwapokea viongozi wetu. Inaniuma sana yale wanayotangaza mikutanoni ni tofauti na uhalisia wa viongozi wetu. Hawa hawajashika dola, wanaongoza kwa kutanua kupitia ruzuku ya walipa kodi,wakishika dola itakuwaje???
Uongozi wa juu, hautaki kututhamini tuliyopo mikoani (Nje ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro); ruzuku haifiki, ofisi za wilayani zina madeni ya kutisha. Semina elekezi zinapelekwa Arusha, Manyara na Kilimanjaro wanakotoka viongozi wa juu. Mie nawashangaa elimu ya viongozi wangu jinsi wanavyoitumia; walitakiwa watumie nguvu na raslimali nyingi katika maeneo ambayo chama hakijajikita badala ya kutumia nguvu nyingi kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. NAWAKILISHA KWA DR. SLAA AJITAZAME AKIWA NI MTENDAJI MKUU WA CHAMA CHETU, chama kipunguze kutumia muda na fedha nyingi katika mikoa ya Kaskazini; tuelekeze nguvu mikoa ya Pwani na Kusini kuna fursa ya kupata wafuasi na wapiga kura CCM huko iko ICU, tusije wapa CUF ujiko.
Ni ushauri wangu,
Mkereketwa wa Chadema,
Lushoto
 
Karibu sana JF ila unafiki uache, hapa ni GT, hizi taarabu ungepeleka nyumbani kwenu zingekusaidia,
Naona kila siku unafungua ID mpya, kwa maneno yale yale, kwa wakati tofauti, pole sana
 
Jitazame kwanza wewe kamanda uliepewa chochote na Makamba junior
 
Kulikua na haja gani kutuambia?au unaona raha kukopost.......aya tumekusikia basi.
 
Wazo lako ni zuri saana Kiongozi, ila lugha iliyotumika haina staha hata kidogo. Nafikiri wahusika watayafanyia kazi na mengine yanaendelea kufanyiwa kazi na uongozi. Pamoja tujenge Chama
 
Sisi wana Chadema tuwe kitu kimoja, mawazo yangu nimeyaweka hapa JF kwa vile kwenye vikao vya chama udikteta upo mbele

Majanga, umefukuzwa CDM, umehamia MaCCM, lakini kutwa kuzungumza ya CDM. Mliberali majanga
 
Tunakukaribisha Mbozi tusherehekee KIFO cha CHADEMA kilitokea jana, mazishi ni leo, mjini WAWA
 
kosa kukosa chama chao tu pole kwa mitusi ndugu yangu utayoyapata lkn ndio usijali
 
Nibora CHADEMA kuliko ccm walio wachafu wa mwili, roho, matendo,na maneno yao!!
 
chama cha wahuni na watembea na sumu mfukoni ata wakienda bar wanazo
 
Kachukue bahasha yako Lumumba.

Hii ni famous quote hapa kwa wale wanaokosoa chama kitakatifu.
 
Waungwana nawasalimia kutoka mashamba ya chai, nipeni nafasi ya kunisikiliza; CHADEMA ni chama kinachonivutia kwa maneno mazuri ya Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe; kinadharia wana kila sababu ya kupewa nchi.


Hata sisiem wanasema hivi!... Lakini usiku kucha wanapanga mbinu za kuhujumu harakati hizi.

Hatahivyo nimejiunga nacho ndipo nikakuta hali tofauti ndani ya chama wala hakina dhamira ya kuchukua nchi. Matendo ya viongozi waandamizi yanaashiria hawako tayari kuchukua dola 2015, badala yake wametanguliza matumbo yao mbele.

Hela zipi zimeliwa?...

Walipofika Lushoto mwaka 2010 kipindi cha kampeni nilijitolea kwa hali na mali kuwapokea viongozi wetu. Inaniuma sana yale wanayotangaza mikutanoni ni tofauti na uhalisia wa viongozi wetu.

Sijui kama kweli uyasemayo umeyatimiza. Huu ni uzushi. Ni kiongozi gani wa Lushoto umeongea naye. Lete jina tuwasiliane naye.


Hawa hawajashika dola, wanaongoza kwa kutanua kupitia ruzuku ya walipa kodi,wakishika dola itakuwaje???

Ndesamburo, Lema, Mbowe n.k wanatumia kodi uliyotoa wewe?


Uongozi wa juu, hautaki kututhamini tuliyopo mikoani (Nje ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro);

Hizi tuhuma ulizitoa hata kabla hujaenda NCCR... Jiulize kaskazini kuna nini?.. Viongozi wengi wa CCM na mawaziri wakuu wametoka huko - mfano Sokoine, Cleopa Msuya, Sumaye, Lowasa, Mrema (Naibu waziri mkuu)..
Nccr Mageuzi - Mbatia - kaskazini..


Sasa shutuma hizi unatoa wapi? Baki NCCR tuachie CHADEMA.

ruzuku haifiki, ofisi za wilayani zina madeni ya kutisha.

Ofisi ipi iliyo na madeni? Ni kiongozi gani wa wilaya ambaye hajui chadema inafanya nini?.. Mimi ni Mwenyekiti wa wilaya ya Bagamoyo. Tulikaa vikao na kuamua mambo ya kufanyia fedha za chama. Ni mwanachama gani usiyejua ukweli huu?!

Semina elekezi zinapelekwa Arusha, Manyara na Kilimanjaro wanakotoka viongozi wa juu.

Hizi semina elekezi ni wewe unazipeleka ARUSHA? na wewe uko CCM?... Kama ni semina elekezi zilifanyika ngurdoto na Dodoma na kuongozwa na mwenyekiti wa CCM.

Mie nawashangaa elimu ya viongozi wangu jinsi wanavyoitumia; walitakiwa watumie nguvu na raslimali nyingi katika maeneo ambayo chama hakijajikita badala ya kutumia nguvu nyingi kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Hivi ungekuwa umefadhili harakati hizi si ungeligawa taifa kwa ukabila wako na ukanda?

NAWAKILISHA KWA DR. SLAA AJITAZAME AKIWA NI MTENDAJI MKUU WA CHAMA CHETU, chama kipunguze kutumia muda na fedha nyingi katika mikoa ya Kaskazini;

Huu uzushi!

tuelekeze nguvu mikoa ya Pwani na Kusini kuna fursa ya kupata wafuasi na wapiga kura CCM huko iko ICU, tusije wapa CUF ujiko.


Hili wazo zuri lisingebebwa na ushabiki wa PM7 aka masalia na pesa za masalia.

Ni ushauri wangu,

Nakutumia namba yangu kwenye private meseji kama una maswali uulize!...

Mkereketwa wa Chadema,
Lushoto

Hakuna mkereketwa wa chadema Hapa. Hivi huko NCCR wamekufukuza?.. Mpaka leo bado unaota CHADEMA?
 
shauri mzuri sana,,,ila jinsi ulivyo present unatia mashaka...
 
Waungwana nawasalimia kutoka mashamba ya chai, nipeni nafasi ya kunisikiliza; CHADEMA ni chama kinachonivutia kwa maneno mazuri ya Dr. Slaa na Mheshimiwa Mbowe; kinadharia wana kila sababu ya kupewa nchi. Hatahivyo nimejiunga nacho ndipo nikakuta hali tofauti ndani ya chama wala hakina dhamira ya kuchukua nchi. Matendo ya viongozi waandamizi yanaashiria hawako tayari kuchukua dola 2015, badala yake wametanguliza matumbo yao mbele. Walipofika Lushoto mwaka 2010 kipindi cha kampeni nilijitolea kwa hali na mali kuwapokea viongozi wetu. Inaniuma sana yale wanayotangaza mikutanoni ni tofauti na uhalisia wa viongozi wetu. Hawa hawajashika dola, wanaongoza kwa kutanua kupitia ruzuku ya walipa kodi,wakishika dola itakuwaje???
Uongozi wa juu, hautaki kututhamini tuliyopo mikoani (Nje ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro); ruzuku haifiki, ofisi za wilayani zina madeni ya kutisha. Semina elekezi zinapelekwa Arusha, Manyara na Kilimanjaro wanakotoka viongozi wa juu. Mie nawashangaa elimu ya viongozi wangu jinsi wanavyoitumia; walitakiwa watumie nguvu na raslimali nyingi katika maeneo ambayo chama hakijajikita badala ya kutumia nguvu nyingi kwenye mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro. NAWAKILISHA KWA DR. SLAA AJITAZAME AKIWA NI MTENDAJI MKUU WA CHAMA CHETU, chama kipunguze kutumia muda na fedha nyingi katika mikoa ya Kaskazini; tuelekeze nguvu mikoa ya Pwani na Kusini kuna fursa ya kupata wafuasi na wapiga kura CCM huko iko ICU, tusije wapa CUF ujiko.
Ni ushauri wangu,
Mkereketwa wa Chadema,
Lushoto

Wewe weeeeee hatudanganyiki, wewe kachukue mshiko wako wa propoganda LUMUMBA. Watu wazima hawaongei porojo, Kama Chandema wako kama unavyosema tafakari yafuatayo:
1. bandari mpya Bagamoyo wakati ya Mtwara na Tanga zinateketea
2. EPZ BAGAMOYO
3. Gesi BOMBA LINAKWENDA BAGAMOYO,
4. Vyuo na matawi ya IFM Bagamoyo
5. Barabara ya kwenda Kaskazini Bagamoyo
6. Wajumbe wa Halmashauri Kuu Riz1 na Mama S
Kwa leo naishia hapa,

Tafakari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kachongee kwa Mamako yawezekana akakuelewa, lakini sisi hatudanganyiki! Chadema na sisi, sisi na chadema mpaka Magogoni tukapange jengo lili 2015. Acha upuuzi wako, rudi kwa magamba wenzako, potezea.
 
Back
Top Bottom