Mapenzi yanaumiza

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,322
Wakati mwingine mapenzi yanaumiza sana. Haswa unapopata mtu ambae sio sahihi kwako. Ambae amekutumia na alichopata alichokua anakitaka kutoka kwako sasa kakipata amekitumia had amekinai au ulichokua nacho sasa kimeisha na yeye mapenz yameisha anaenda kwa mwingine. Kumbe masikin ya Mungu mwenzio alikua na mapenz ya dhati kwako. Laana nyingine mbaya sana.

Niliwahi kushuhudia mahubiri ya Prophet Bushiri nadhan kwa ambao hua mnamfuatilia mtakua mnamjua, katika ibada yake moja alivomaliza kuhubiri akaanza kuwaombea baadhi ya waumini akaja kwa dada mmoja akamuita mbele, akamuambia wewe una matatizo makubwa dada anamjibu ndio huku anaanza kulia, Bushiri anamuambia huna amani katika ndoa yako, hujapata mtoto, mumeo anatembea na wanawake wengine, na ni mlevi, na anakunyanyasa...anamuuliza "am i right?" .dada akamjib kwa saut huku bado analia kua yote ni kweli, kwamba ammsaidie , prophet bushiri anamuuliza unajua sababu ya haya yote ni nini?

Mwanamke yuko kimya,..kama kawaida yake Bushiri hua anazunguka kwanza kama dakika 3 halaf anaanza kucheka, ...ghafla anamuuliza yule dada .."unamfahamu fulani(jina), anataja jina la mwanaume....
yule dada anashtuka ...bushiri anamuambia kua huyo kaka lazima atafutwe ila kwa nguvu za binadam sio rahis lakin nitaomba na Mung atamleta mwenyewe hapa kanisan ...

akazid kumwambia kua huyo kaka alikua na mahusiano nae na huyo kaka alimpenda sana lakin badae akamuacha na kwenda kwa mwanaume mwingine ambae ndo huyo anaeish nae, akamwambia tu kwa kifupi, "that your x lover cursed you, he was hurt and he cursed you" yaan alimlaani na kuivunja ile laana lazima kijana atafutwe ili umuombe msamaha na maombi yafanyike ili uweze kufunguliwa....dada huku anapiga yowe...akamwambia tu wampeleke ofisin kwake kwa ajil ya maongez zaid mana kuna mambo mengine ni ya ndani sana na ni ya kifamilia.

Nilichojifunza ni kwamba usimfanyie mtu kitu kitakachomuumiza ambacho wewe hutapenda kuja kufanyiwa hicho hicho. Wakati mwingine mambo tunalia kua hayaendi mara unalalamika ndoa chungu ama mahusiano machungu ama unanyanyaswa lakin ukija kuchimbua unakuta kuna mtu ulimfanyia hivyo.hivyo kumbe sasa inakujeukia yaani KARMA inatimiza kazi yake sasa kwa wakati huo.

Kwa leo niishie hapa.

FB_IMG_1484569866939.jpg
 
Nilichojifunza ni kwamba usimfanyie mtu kitu kitakachomuumiza ambacho wewe hutapenda kuja kufanyiwa hicho hicho. Wakati mwingine mambo tunalia kua hayaendi mara unalalamika ndoa chungu ama mahusiano machungu ama unanyanyaswa lakin ukija kuchimbua unakuta kuna mtu ulimfanyia hivyo.hivyo kumbe sasa inakujeukia yaani KARMA inatimiza kazi yake sasa kwa wakati huo.
ndicho ninachoamini
kila unalofanya lina malipo yake..
ukitenda jema, utalipwa jema
ukitenda baya, utalipwa baya
hapa hapa duniani..! sio kwingine.
 
Hili limekaribia kunikumba a have a lot of stress. Nilitaka kuomba ushauri nikasema nivumilie kidogo. kifupi Nina mahusiano na binti wa dini tofauti lakini tunapendana sana na mwaka huu nilipanga panapo majaliwa tuoane. tatizo Mwenzangu anataka Mimi nibadili dini nimfuate yeye, na hofu kubwa aliyonayo yeye kwao wanataka ndoa ya kiislam tu hawataki abadili wala hawataki ya serikali. na hivi karibuni amepata shinikizo na ameanza kubadilika na kuwa na msimamo mkali kuwa nibadili dini mimi kama sitaki tuachane. na Nina miaka zaidi ya 3 tupo kwenye relation na hatujawahi gombana kufikia hatua ya kutamani kuachana. sasa nina mtihani mkubwa hata jibu silipati yote ninayojaribu wazee wake wa imani kali anaogopa kutingwa. na Mimi sipo tiyar kamfuata mwanamke dini yake coz naamini katika dini yetu. ila tunapendana Sana Sana naomba ushauri wa kujenga please and please wadau.
 
Unampataje mtu ambae sio sahihi kwako?
Kwani mwanzon utajua nini?? Mnakutana unampenda na yeye anakuonesha anakupenda lakin kumbe ni uongo na mwisho wa siku kitu alichokua anakihutaji ameshakipata ama alichokua anakipata kutoka kwako kila akiwa na shida kimeisha bas na mapenzi yanaishia hapo na ndo utakuta ugomvi usioisha na kutafuta sababu alimradi muachane apate kwenda kwa mwingine. Kwaio wewe ni kama alikutumia tu. Umenipata sijui
 
Nilitaka kuanza Uzi ila naona umwgusa yale ambayo nilitaka kuyasemea..

Uliyosema ni kweli,kweli kabisa.... Na ndomana ndoa nyingi hazidumu kutokana na hizo KARMA ambazo tunafanyia wengine
Valentina hivi vitu vipo sem watu hua wanachukulia simple sana, lakini vikija kufumuka kama vilivyofumuka kwa huyo dada wa kwa Prophet Bushiri unakuta its too late and the damage has been done
 
Hili limekaribia kunikumba a have a lot of stress. Nilitaka kuomba ushauri nikasema nivumilie kidogo. kifupi Nina mahusiano na binti wa dini tofauti lakini tunapendana sana na mwaka huu nilipanga panapo majaliwa tuoane. tatizo Mwenzangu anataka Mimi nibadili dini nimfuate yeye, na hofu kubwa aliyonayo yeye kwao wanataka ndoa ya kiislam tu hawataki abadili wala hawataki ya serikali. na hivi karibuni amepata shinikizo na ameanza kubadilika na kuwa na msimamo mkali kuwa nibadili dini mimi kama sitaki tuachane. na Nina miaka zaidi ya 3 tupo kwenye relation na hatujawahi gombana kufikia hatua ya kutamani kuachana. sasa nina mtihani mkubwa hata jibu silipati yote ninayojaribu wazee wake wa imani kali anaogopa kutingwa. na Mimi sipo tiyar kamfuata mwanamke dini yake coz naamini katika dini yetu. ila tunapendana Sana Sana naomba ushauri wa kujenga please and please wadau.
Haya mambo ya dini haya wakati mwingine hata msilazimishage sana mambo,inaweza kuja kuwacost.
 
Ni uamuzi mgumu kama haupo tayar kumfuata inabidi muachane tu maana akija dini yako lazima atabeba ile lawama toka kwa familia yake,na wewe hivyo hivyo utabeba kinyongo toka kwa familia yako. ILA WAKATI MNAANZA UHUSIANO SI MLIJUA MNA DINI TOFAUTI MLIELEWANAJE KUHUSU SUALA HILO?

ushasema huwezi fuata dini ya mpenzi wako........kwanza mnaelewa maana ya dini kweli?? Mshafanya uasherati kwa miaka 3..... leo hii unathubutu kusema dini zinapingana...... hampendani nyie ....... tamaa za ngono tuuu.....Ongea na Muumba wako... kama ni sahihi kuwa wako... dini haiwezi kuzuia kitu.... pole sana.
 
Tulijua dini tofauti lakini tulikubaliana kuwa na ndoa ya serikali lakini mazingira ya kwao alivyoyasoma ni magumu kukubali. that's why inakuwa hivyo but we real love each other. tatzo imani
 
kuwa na mahusiano sio kufanya uasherati mkuu acha kejeli kama huna ushauri Kaa kimya nahitaji mawazo ya kujenga sio maneno ya hovyo hovyo.
 
Poleni. Jiulize moyoni kama waweza muachia aende kwa amani bila kuweka kinyongo.kama waweza mwache aende,(kuna wengine ili kulazimisha ndoa wanapeana mimba kwanza huu uamuzi huwa una madhara sana.)

dada yako huyo.........wacha kujifanya malaika wewe..... Tubu Mrudie Mungu wako mwambie mahitajio yako .....bwege wewe......umeshindwa kulitatua huko hapa tunakushauri na kukusukumia kule.....akili mbovu sana...
 
Poleni. Jiulize moyoni kama waweza muachia aende kwa amani bila kuweka kinyongo.kama waweza mwache aende,(kuna wengine ili kulazimisha ndoa wanapeana mimba kwanza huu uamuzi huwa una madhara sana.)
Asante nishafikiria hiyo plan ndo tuifanye ila challenges will arise still japo pengne zenye mlengo tofauti. but sote hatupo vzur kwa Kweli tunahali ngumu tushazoeana Sana kiukweli.
 
Back
Top Bottom