Mapenzi yanauma sana

Mapenzi yanauma sana

Sasa ipo ivi kipindi naanza chuo nilikutana na mdada mmoja tunasoma course moja tukazoeana lecture tukawa tunakaa wote namsainia na kumfanyia assignment asipokuwepo kiukweli ule ukaribu ulinifanya nimpende Sana but sio mzuri sana

Tuna karibia kumaliza first year nikamtongoza akachomoa na kuniambia yeye ana boyfriend apo chuoni wa course nyingine japo ni first year

Sikukata tamaa nikafanya survey nikajua kweli anae but jamaa hampendi ila demu anamganda hiyo ikanipa moyo tukaendelea ivo ivo na ukaribu wetu mda mwingi nakuwa nae tunaenda coco beach maana hostel zipo karibu na coco

Second year nikakomaa tena lakn nikagonga mwamba nikaamua ku give up but akawa mda wote ananitafuta niliendelea kumkwepa ilikuwa rahis kumkwepa maana m nilianza kuishi geto
Tatizo likanza magroup mengi tukawa tunapangwa wote kwahyo kumsahau nikashindwa tukaendelea tena kuwa karibu nikamtongoza akapotezea tena

Tukiwa mwaka wa mwisho tukapagwa field group moja huko kijijini wanawake Kumbe yule demu kuna mshikaji mwingine wa class anamla ubaya yule mshikaji chumba chake na changu vilikuwa karibu alaf ceiling board imetoboka sana kias kwamba sauti nazisikia niliumia sana na sidhan km nishaumiaga km kipind hicho wakati wa kula wanalishana wakawa km wananikomoa na huyo mshikaj alikuwa anajua kabisa kwamba me nnasota pale
Kibaya zaidi yule mshikaji ana mademu watatu wazuri Sana kuliko huyo na alikuwa anamla kwasababu yupo mbali na madem zake

Nilipitia kipind kigumu sana mawazo yakanizid sana nikawa natumia mda mwingi kulala nikaji isolate na group members nikajitahid kusikiliza Sana nyimbo nakumbuka wimbo wa Juice world LUCID DREAM ndo niliusikiliza Sana hatimaye field ikaisha

Tulivyorudi chuo nikafuta namba zake na kukata mazoea kabisa tukikutana bahat mbaya tunasalimiana basi
Tukafanikiwa kumaliza chuo kila mtu akarudi kwao akawa ananitafuta ananiambia amenimiss namjibu asante
Naapa kabisa namchukia Sana huyo mwanamke
Pole sana Mkuu

Nafeel jinsi unavyofeel right now.

Hali kama hiyo imeshatutokea wengi tu, we we si wakwanza. Lakini ujue kuwa yawezekana Mungu amekuepusha na matatizo ambayo ungeyapata kama ungekuwa nae kimahusiano.

Jipe moyo utampata mwingine mzuri zaidi na utamsahau huyo.
 
Asante sana mkuu at least comment yako inafariji maana wengine wanachojua wao ni crash
 
Umenikumbusha Allen wa chuo, alinipenda sana huyu kaka ila sikumuelewa kipindi kile. Nakumbuka alipanga twende out beach mimi na yeye tuu siku nzima, nikamkatalia na mitongozo yake yote nilimtolea nje. Alipomaliza chuo aka give up, siku moja miaka kadhaa baada ya kumaliza chuo tukakutana, akanisimilia mengi jinsi alivyokuwa anaumia kunikosa nikajikuta napata uchungu mkubwa kuzidi aliopata akiwa chuo.

Tukaagana kwa denda moja takatifu, tangu hapo hatujaonana tena.

K’ Matata.
Allen mzembe..Hakukumbuka kuchukua hata namba..
 
Allen mzembe..Hakukumbuka kuchukua hata namba..

Aahahahhahaaa alikuwa mkatoliki safi sana, alipata mafunzo ya seminarini ila baada ya kumaliza chuo anasema alikuwa player mno sababu ni mimi kumkataa.

Hakuchukua namba sababu bado alikuwa ananipenda na hakutaka kuniumiza maana wakati huo alishakubuhu kwenye u player kiasi kwamba anakanyaga kanyaga....

Ni wanaume wachache sana wanajali...
 
baharia unafeli kimisingi..... mbona sie tumekataliwa sana we kwani wa kwanza...afu mwanaume kuchukia huo ni upimbi
 
Umenikumbusha Allen wa chuo, alinipenda sana huyu kaka ila sikumuelewa kipindi kile. Nakumbuka alipanga twende out beach mimi na yeye tuu siku nzima, nikamkatalia na mitongozo yake yote nilimtolea nje. Alipomaliza chuo aka give up, siku moja miaka kadhaa baada ya kumaliza chuo tukakutana, akanisimilia mengi jinsi alivyokuwa anaumia kunikosa nikajikuta napata uchungu mkubwa kuzidi aliopata akiwa chuo.

Tukaagana kwa denda moja takatifu, tangu hapo hatujaonana tena.

K’ Matata.
Uchungu mkubwa kuzidi aliopata akiwa chuo. Ulitumia mizani gani mkuu kujua wako ulikuwa mkubwa kuzidi wake kipindi cha chuo?
 
Uchungu mkubwa kuzidi aliopata akiwa chuo. Ulitumia mizani gani mkuu kujua wako ulikuwa mkubwa kuzidi wake kipindi cha chuo?

Tuliongea mambo mengi sana sijayaelezea hapa, alifungika vitu vingi sana ambavyo akiwa chuo hakuniambia. Niliupata uchungu wake kwenye mazungumzo ya siku hiyo na baadae ya hapo uzito na maumivu niliyoyasikia naona aliyopitia yeye wakati ananitongoza ilikuwa cha mtoto.
 
Back
Top Bottom