Mapenzi yanauma jamani...

Mapenzi yanauma jamani...

Mapenzi ni sawa na yai na kuku nani wa kwanza kuzaliwa
 
Pole sanaaa. Ukipenda kwa moyo wako wote na penzi linapofikia ukingoni lazima uumie sana. Itachukua muda maumivu unayoyapata sasa hivi kupotea, lakini usiogope kupenda tena kwa moyo wako wote na akili pia kwa kuogopa kuumizwa.



Hivi kuna siri gani nyuma ya mapenzi. Kwanini mapenzi yawe yanauma sana? and when love is over, where does it go?!!
 
Mwenye pesa akigundua hapendwi yeye bali inapendwa pochi nene AKA pesa itakula kwake mpenda pochi nene.

Penda pesa hautaumia ukimpenda mtu tutakuimbia parapanda soon
 
lol! lazima tu ujinasue 🙂🙂 akishazisaka na kuzipata kutumia pekee yake hazinogi kama hana wa kujidai naye kashika kiuno kwa raha zake na za msakapesa.

Sio lazma kupenda pesa za mtu ila kupenda tu pesa in general, kuzisaka, kuzitumia....
 
tafuta pesa dada usimtegemee mwanaume kama unahitaji kuwa na maisha yako
 
Katika maisha kuna mambo mawili ambayo yamefanikiwa kumletea mwanadamu maumivu makali ya moyo. Kufiwa na mtu wa karibu, na mapenzi.

Ukiishi bila kukumbana na hivyo vitu viwili basi utakuwa na raha duniani. Hata kama ni maskini.
 
Usiendekeze mapenzi, usiyafanye kiwa kitu namba 1 ktk akili na nafsi yako, kuuma kuwa kawaida na kutokuuma kabisa ni wewe mwenyewe jinsi unavyojiweko huko. Kuna watu hawajui thamani ya hii kitu ila wanamambo yao yanayowanyima usingizi.
 
Back
Top Bottom