Mapenzi yana nguvu sana

Mapenzi yana nguvu sana

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
20,143
Reaction score
40,910
Habari zenu wakuu.

Nilikuwa sifahamu au kushuhudia nguvu ya penzi, mpaka juzi kati niliposhuhudia live.
Brother wangu aliugua ghafla na chapu chapu tukampeleka zahanati iliyokaribu kwa ajili ya matibabu, lakini kiukweli alikuwa na hali mbaya sana.

Kwa kuwa hata kula ilikuwa taabu maana tulibembeleza mpaka basi maana mtu mzima hamuwezi kumshika mdomo wakati tunafikiria nini cha kufanya nikapata wazo la kumpigia my honey wake.

Wakati huo mgonjwa alikuwa bado yupo usingizini, basi punde si punde shemu akatia timu sasa wakati anaingia huku anatusalimia kumbe bro alikwisha sikia sauti yake na hapo ndipo nilipo shuhudia nguvu ya penzi maana nilimuona bro akijiweka sawa tayari kwa kumpokea mgeni kana kwamba alikuwa amejipumzisha tu.

Ikabidi tumkabidhi shemu ule msosi ambao mgonjwa aligoma kula.

Kufumba na kufumbua kutokana kulishwa na my honey wake chakula chote alikimaliza, jambo ambalo hatukulitegemea kwa hiyo tukabaki na mshangao.

AMA KWA HAKIKA PENZI LINA NGUVU....
 
Kama mtu akiweza kubadili/convert power of love into mechanical or eletrical power then the whole world would be full of light!!
 
alitaka my honey wake amkute mzima amtie moyo
ila kiukweli hata mimi nikiumwa afu ghafla my honey wangu anakuja aisee napata faraja sana
 
Ahaaaaaaaaaaaaa...
Nimegunduwa kitu...
Na mm ntawaambia ndugu zangu nikiugua wawe wanamwita wife wangu kunilisha maana nakuwaga msumbufu sana wa kula...
 
...wakuuu.....
Nilikuwa sifahamu au kushuhudia nguvu ya penzi...mpaka juzi kati niliposhuhudia live...
Brother wangu...aliugua ghafla na chapu chapu tukampeleka zahanati iliyokaribu kwa ajili ya matibabu...lakini kiukweli alikuwa na hali mbaya sana...kwa kuwa hata kula ilikuwa tabu....maana tulibembeleza mpaka basi maana mtu mzima hamuwezi kumshika mdomo....wakati tunafikiria ni cha kufanya nikapata wazo la kumpigia my honey wake....wakati huo mgonjwa alikuwa bado yupo usingizini....basi punde si punde shemu akatia timu...sasa wakati anaingia huku anatusalimia kumbe bro alikwisha sikia sauti yake.....na hapo ndipo nilipo shuhudia nguvu ya penzi...maana nilimuona bro akijiweka sawa tayari kwa kumpokea mgeni kana kwamba alikuwa amejipumzisha tu....ikabidi tumkabidhi shemu ule msosi ambao mgonjwa aligoma kuula....loh!!!...kufumba na kufumbua kutokana kulishwa na my honey wake chakula chote alikimaliza..jambo ambalo hatukulitegemea kwa hiyo tukabaki na mshangao....
AMA KWA HAKIKA PENZI LINA NGUVU....

Kendekezana tu, njaa ingemkaba kisawa sawa na kuona anakaribia kuzimika angekula mwenyewe mbona. Mapenzi ya kwenye TV tabu sanaaa !!! Lol
 
 
Last edited by a moderator:
Penzi penzini !
Kuwa loved and to love aseee ni raha sana!
The feelings that you are cared
asee huoni kama kuna kitu kingine kinaexist!
Not even kuumwa not even kushindwa kula!
Hehehehehehe kuweeeeepo tu pale imempa nguvu ya kula /kunyanyuka/mpk anajiandaa kupokea mgeni!
Asee aaacha bana!
Power of love ya Celine Dion
Isindikize hii post!
Mashairi ya All of Me ya John the Legenf yapeperuke nayo!
Juuust on point!
 
Back
Top Bottom