Mapenzi yaliondoa maisha ya ndugu yangu

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2009
Posts
1,963
Reaction score
2,479
(ANGALIZO HII NI STORY YA KWELI) ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa tisa mnamo saa tatu na nusu usiku taraitibu napiga hatua kuelekea nyumbani mara ghafla simu ikaitwa kuangalia ni ya dada yangu aliyepo morogoro, nikapokea kwa furaha maana sijawahi kuwasiliana kwa muda murefu, maskini kuona tu dada anaongea kinyonge furaha ikaniisha ghafla, kumsikiliza ndo akaniambia habari za kuhuzunisha kuwa mdogo wangu amekutwa amekufa.

ninayemwongela hakuwa mdogo wangu tumbo moja bali alikuwa mtoto wa kwanza wa mama yangu mdogo anayeishi huko kigurunyembe morogoro. baba wa mdogo wangu huyo alifariki miaka mingi iliyopita hivyo mama yangu mdogo ndo alihangaika kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji yake yote ya msingi ikiwepo elimu. mdogo wangu huyo mauti yalimfika huku zikiwa zimebaki siku tatu kuriport chuo cha mzumbe tawi la mbeya alikokuwa amechaguliwa kusomea masomo ya sheria kwa ngazi ya degree.

MAZINGIRA YA KIFO
mdogo wangu siku ya tukio aliaga anaenda kwa bibi yake kuchukua baadhi ya mahitaji kwa ajiri ya safari ya kwenda chuoni, inavyosemekana alipokuwa akirudi ndipo alipotekwa na vijana ambao hatujui idadi yao na kwenda kumuua na kisha kumtupa barabarani.
KWA NINI ALIUWAWA
Inavyosemekana mdogo wangu alikuwa ana uhusiano na binti mmjoa lakini baba yake kumbe hakufurahishwa na uhusiano huo wa mwanawe na mdogo wangu huyo hivyo basi akaamua kumtumia vijana ili wayatekeleze mauaji yale

NANI ANATUHUMIWA
mtuhumiwa wa mauaji yale bila kuficha ni ni DIWANI MMOJA KATA NIMESAHAU PALE MOROGORO MJINI AMBAYE NIMEFANIKIWA KUTAJIWA JINA LAKE MOJA ANAITWA KIMARO ( KWA WALE WAKAZI WA MOROGORO WATAKUWA WANAMFAHAMU HUYU)

JE KESI INAENDELEAJE
Baada ya kutuhumiwa kwa haya mauaji huyu diwani alikamatwa lakini aliachiwa baada ya muda mfupi bila sababu maalum, ndugu zangu waliopo morogoro walipojaribu kuhoji walipewa vitisho na askari polisi hivyo basi kama familia walikaa kikako wakaamua wamwachie mungu maana wao kama wao hawakuwa na uwezo wa kushindana kipesa na diwani huyo ambaye inasadikika alitumia pesa kutoka

KWA NINI ATUHUMIWE DIWANI KIMARO
diwani huyo alituhumiwa baada ya kutajwa na wale vijana ambao wanasemekana walitekeleza mauaji hayo, kumbuka damu ya mtu ni nzito maana siku ile ile ya msiba kuna kijana alikuja kufuatilia mauaji waliyoyafanya, kijana huyo alikamatwa na akawataja wenzie ambao kwa pamoja walimtaja diwani kimaro.

HIVYO NDIVYO MAPENZI YALIVYOMTOA UHAI MDOGO WANGU, BABA WA BINTI KWA SABABU ALIKUWA HAMTAKI MDOGO WANGU NDO AKAAMUA AMTUMIE WAUAJI AMBAO BILA WOGA WALIMUUA NA KUMTUPA BARABARANI
MUNGU AMLAZE MDOGO WANGU HUYO MAHALA PEMA PEPONI AMENI


Nashukuru mkuu kwa mchango wako pia naomba nikusahihishe kidogo ni kuwa mwili wa marehemu uliokotwa siku iliyofuatwa wakaitwa polisi kisha akaitwa mama wa mtoto ukatambuliwa kisha tukauzika wenyewe
 
Ndo tz yetu! Watu wako juu ya sheria!! Pole sana!
 
KAma ni habari ya ukweli mkuu kwa nini usiende Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu watakupa msaada wa kufuatilia jambo lako maana ni kesi ya mauaji mkuu na uhai umepotea wa mdogo wako kwa visa vya ajabu
Na hata Tume ya haki za Binadam na Utawala Bora unaweza kupeleka shauri lako mkuu Maana wako pale kusaidia watu kama wewe ambao mna madai ambayo yameacha yaishe bila msaada wowote
Usikae kimya wakati kuna uwezekano wa haki ya mdogo wako kupatikana kwani huwezi kuuondoa uhai wa mtu kisa hutaki binti yako apendane na mtu mfungie ndani basi asitoke kabisa aishi kwenye ulimwengu wa peke yake
 

MR ROCKY nimekuelewa, unajuwa mimi wakati huo mwaka juzi nilikuwa masomoni kwa hiyo iliniwia vigumu hata hivyo sikujua hayo yote, hata hivyo nilijiapiza kuwa ntahakikisha dunia inajua udhalimu huu kwa njia yoyote ile maana huko mahakamani sikuwa na uwezo wa kumshitaki maana yeye ana pesa
 
Apumzike alietangulia mbele ya haki lakini seem umesukumwa na hisia zaidi kutuhumu mtu kihisia....
 
mnyikungu kusanya ushahidi wote ambao unaweza kuupata na nenda kweney sehem nilizokuambia hapo juu wasilisha ushahidi wako na vielelezo vyako na watakupa ushauri tena wakati mwingine hata bure watakupa na mwanasheria wa kusimamia issue yako
Usikubali tuu haki ya mdogo wako ipotee au dam yake ipotee kisa kuna mtu mwenye pesa ameamua iwe hivyo
 
Last edited by a moderator:
Apumzike alietangulia mbele ya haki lakini seem umesukumwa na hisia zaidi kutuhumu mtu kihisia....
ndo maana hapo nimesema anatuhumiwa, sijamlenga moja kwa moja maana mamlaka ya kufanya hivyo ni mahakama pekee
 
Kama mambo ni hivyo hapo morogoro mjini kwenye watu wenye uelewa wa sheria je huko vijijini niaje?
So sad, nchi hii tunakoelekea ni kubaya zaid, kama ni kweli mtu anaamlisha mtu auwawe na anauwawa. mh haijakaa sawa kabisa!
 
Aisee hii stori inatutoa kwenye mada ya mapenzi na kutupeleka kwenye murder case(tuhuma) ,matabaka kati ya walionacho na masikini tatu above the law,kwamba kuna watu wako juu ya sheria

ESent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Pengine huyo binti alikuwa 'mtoto wa baba' maana mijianaume mingine hasa kutoka pande.... ni ya hovyo. Siamini kama mzazi anaweza kuwa na wivu kiasi cha kutoa mtu roho kama hana upande wa pili.
 
Pole sana. Mambo hayo yanatokea sana hasa sehemu za mjini ila wahanga wanakuwa hawajuhi wafuate utaratibu gani ili haki itendeke. Fuata ushauri uliyopewa ili mpata haki katika hili.
 
Pengine huyo binti alikuwa 'mtoto wa baba' maana mijianaume mingine hasa kutoka pande.... ni ya hovyo. Siamini kama mzazi anaweza kuwa na wivu kiasi cha kutoa mtu roho kama hana upande wa pili.

hata mimi nilitaka kusema hivyo hivyo
 
Pengine huyo binti alikuwa 'mtoto wa baba' maana mijianaume mingine hasa kutoka pande.... ni ya hovyo. Siamini kama mzazi anaweza kuwa na wivu kiasi cha kutoa mtu roho kama hana upande wa pili.
dada hawa wapenzi walikuwa na rika sawa kabisa wote walikuwa above 20, so huyo baba aliamua tu kufanya hivyo kwa sababu anazozijua yeye
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…