mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
Mapenzi ya siku hizi tofauti na zamani Ya sasa yanahirinzi,au kitanzi shingoni Mapenzi ni kama wizi,ulahai wa moyoni Wapendwao si wajuzi,hawajui kuthamini Wengi wao ni bazazi,mapenzi ya mdomoni Wamekua km nzi,haweshi vichochoroni Nami nasema siwezi,hili penzi la kihuni Wanifanyia ushenzi,eti unanitahini Takuona mpuuzi,kama hujajibaini Kila ninavyokuenzi,hujui yangu thamani Nenda kwa hao washenzi,wakulao majini