mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
Mapenzi ya siku hizi tofauti na zamani
Ya sasa yanahirinzi,au kitanzi shingoni
Mapenzi ni kama wizi,ulahai wa moyoni
Wapendwao si wajuzi,hawajui kuthamini
Wengi wao ni bazazi,mapenzi ya mdomoni
Wamekua km nzi,haweshi vichochoroni
Nami nasema siwezi,hili penzi la kihuni
Wanifanyia ushenzi,eti unanitahini
Takuona mpuuzi,kama hujajibaini
Kila ninavyokuenzi,hujui yangu thamani
Nenda kwa hao washenzi,wakulao majini
Ya sasa yanahirinzi,au kitanzi shingoni
Mapenzi ni kama wizi,ulahai wa moyoni
Wapendwao si wajuzi,hawajui kuthamini
Wengi wao ni bazazi,mapenzi ya mdomoni
Wamekua km nzi,haweshi vichochoroni
Nami nasema siwezi,hili penzi la kihuni
Wanifanyia ushenzi,eti unanitahini
Takuona mpuuzi,kama hujajibaini
Kila ninavyokuenzi,hujui yangu thamani
Nenda kwa hao washenzi,wakulao majini