Dada yangu mimi aliolewa na mwanaume aliefahamiana nae instagram tokea yupo chuo mwaka wa pili UDSM so kipindi anarudi likizo hom alikuwa hanifichi kuhusu hilo kuwa amepata boyfriend kutoka instagram
Lakini hiyo ilikuwa ni siri yetu sisi tu hadi anamaliza chuo mwaka 2016 na ndoa wakafunga kabisa lakini siri ilibaki kuwa moja tu je Walifahamiana wapi ?
Hilo ndio swali ambalo ilibidi wadanganye kwa wazazi kuwa hawakufahamiana kwenye mtandao bali walikutana kipindi sister yupo field kwenye kampuni flani hivyo ndio mahusiano yakaanzia hapo, ilibidi wadanganye hivyo ili kuondoa wasiwasi kwa wazazi
Ila tu sio kila unayemuona kwenye mtandao umuamini direct........