Mapenzi ya media/wahariri na utawala huu wa awamu ya tano yananipa mashaka sana

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,670
149,840
Hivi mtu aliesoma kozi ya journalisim na kufuzu vizuri anaweza kufanya kazi ya uandishi kwa style hii ya vyombo vyetu vya habari vinavyofanya kuhusiana na utendaji kazi wa awamu hii?

Hivi huu uandishi ni matokea ya kuwa na nidhamu ya woga au kuna kitu waandishi wetu wanakitafuta?

Je,hawa waandishi kweli wako neutral?

Hivi bado tuko kwenye kampeni au ndio tumeanza kampeni za kuelekea 2020?

Nijiuavyo mimi ni kuwa,mwandishi anatakiwa awe objective ili mlaji wa habari mwenyewe ndio afanye maamuzi sahihi juu ya jambo linaloripotiwa na si kumjengea mazingira ya kumshawishi kuwa serikali hii ni nzuri au vinginevyo.Sasa je,hiki ndicho waandishi wetu wanachokifanya kwa sasa(kutokuwa na upande)?

Jamani nawapa homework mjaribu kufanya tathimini ya jinsi media zetu zinavyoripoti habari zinazohusu awamu hii ya tano kwa kuzingatia misingi ya taaluma ya uandishi wa habari muone kama waandishi wetu wanazingati walichofundishwa huko vyuoni.

Assignment ya kwanza:Chunguza heading zote za magazeti ya kesho na siku mbili au tatu zinazofuata.

NB:Kuna vyombo vichache sana vimebaki kusimamia misingi ya taaluma ya uandishi ila vingine vingi mimi sina imani navyo kabisa.
 
Pasco wala asiwaumize kichwa maana huyo ndio kabisaa hii fani imemshinda
 
Fatilia kwa kina Gazeti la Jamvi la Habari liko makini na la kueleweka kuliko Magazeti mengine yanayofanya kazi kwa kufata uelekeo wa upepo
 
1458243004063.jpg
 
Be more specific!ni kitu gani kinakukera?magufuli kuandikwa zaidi kuliko LOWASA?au kitu gani?movie ya LOWASA imeisha brother! maybe unataka media ireport LOWASA akichunga ngombe?mwenyewe kasema siasa basi.au anzisheni zile movie zenu za maandamano mnaweza pata coverage !
 
Tujiulize Rais anapokuwa 'anauza magazeti'
kuliko wacheza filam....nini maana yake?

halafu Rais huyu huyu anaenda kupiga simu live kipindi cha tv

ana malengo gani?
hajui kweli atazua gumzo?
kama anajua why anafanya?
 
Hili ni mojawapo la gazeti ambalo Mhariri wake anajitambua bila kusahau gazeti la Dira na kiasi fulani gazeti la Rai Mwema.
hahaha kamanda kwahyo hata kubenea na gazeti lake la mwanahalisi nalo huliamini siku hz? maana nape akiyafungia mnakuja kulia huku jamvini yakiachwa na kusifia utendaji wa magufuli mnatokwa povu, acheni wivu bavicha
 
Hivi we jamaa una kimbuka vizuri gazeti la mwanahalisi na chadema? Mawio je?

Vipi uone kosa kwa magufuli...
 
UKAWA huwa mnatia huruma sana vyombo vya habari vikiwa upande wa wawatani zenu..

Siasa za magazeti ndio zinawapumbaza kumbe!!!!
 
Tanzania hakuna waandishi wa habari kuna makanjanja!!!....JK

MTU anayelipwa chini ya laki 3 kwa mwezi unategemea asihudumie tumbo lake kwanza?
 
Be more specific!ni kitu gani kinakukera?magufuli kuandikwa zaidi kuliko LOWASA?au kitu gani?movie ya LOWASA imeisha brother! maybe unataka media ireport LOWASA akichunga ngombe?mwenyewe kasema siasa basi.au anzisheni zile movie zenu za maandamano mnaweza pata coverage !
Uzuri Ilani mlioinadi kwa wananchi haitekelezwi kupitia media hivyo endeeleeni tu na maigizo yenu mkifikiri muda unawasubiri.
 
Back
Top Bottom