Mapenzi ya huruma...

Nikakumbuka ambavyo sijawahi onewa huruma na niliyempenda,sinaga huruma na mtu...hivyo tu
 
Na kwanini umuonee huruma yeye na si wewe mwenyewe...huoni unajiumiza..??!! ..binafsi siwezi kukuonea huruma maana nahisi nitateseka tu kwenye hayo mahusiano.
 
Hivi mtu alishawahi kutokewa na hii kitu yaani unapenda mtu kwa kumuonea huruma yaani humpendi ila huruma ila kutokana kumuonea huruma unamkubali tu?
Nakuelewa ulichomaanisha ila tatizo maelezo yako hayatoi picha halisi ya mapenzi ya huruma.

Mapenzi ya huruma yapo, ila yanatokea yakitegemea sana mazingira ya wahusika. Mfano unakuta binti amefiwa na wazazi pengine wote na hana faraja, unakuta faraja yake ni Kijana maana ndie aliyekaribu nae. Mazingira ya kumhani, kumbbeleza pengine analia, sijui utamduta machozi, mara utamhug kwa muda fulani ukiwa na nia njema kabisa wala sio mapenzi, hali ya namna hiyo ikikakaa kwa kipindi fulani huanza kuchochea hisia na msisimuko wa kimapenzi na utashangaa katikati ya kumbembeleza na kumpa faraja kama mnavofanya mara zote, mnaanza kufanya mambo kama wapenzi na baadae huanza mahusiano.

Kwa uelewa wangu hayo ndio mapenzi ya huruma. Mazingira hayo ni mfano ila yapo mengine ya kufanana na hayo. Mapenzi mengi ya huruma hayana kutongozana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom