Mapenzi ya dhati yakoje? Yanafananaje?

"Mapenzi ya dhati ni mapenzi ya kweli yatokayo moyoni mwako, ni yale mapenzi ambayo mtu humpenda mtu kwa sababu ya kumpenda, humpenda mtu kama alivyo. Ni aina ya mapenzi ambayo kwa wenyetu walokole huyaita mapenzi ya AGAPE" - hivi ndivyo staff mwenzangu beatrice aliyonijibu pindi nilipo mmuliza swali juu ya maana ya mapenzi ya dhati.
 
Wachangiaji wote vizuri mmetoa michango yenu, lakini nikiangalia naona wengine wamejikita kuelezea kama hayo mapenzi ya dhati yapo au vp.
Mie nianzie kwenye swali lenyewe ambalo ndio topic haswa: Mapenzi ya Dhati yakoje? Yanafananaje?

Ili twende pamoja, muanzisha thread lazima kwanza na wewe tujue una fahamu Mapenzi au umeishawahi kupendwa au kupenda? Kama hilo swali ni gumu basi tupe hata umri wako ili tujue tunaongea na mtu wa level gani katika huu ulimwengu wa mapenzi.

Kwa faida ya wote naanza kama ifuatavyo:

MAPENZI: Ni kitendo au tabia ya kufurahia kufanya au kuwa na kitu fulani(tafsili yangu, ruksa kuangalia Kamusi). Hapa nitazungumzia Mapenzi katika Mahusiano ambayo wengi wetu ndio tunajadili hapa(Mme na Mke); kwamba ni kufurahia kuwa na uhusiano na mtu wa jinsia tofauti na yako, mkishirikiana katika mambo ya kila siku katika maisha, ikijumuisha na mambo ya kujifurahisha au kukidhi mahitaji ya kimwili yanayoshirikisha watu wawili kushirikiana kwa pamoja kama vile tendo la ndoa na kadhalika.

DHATI: Ni kitendo cha kuwa na hiari ya kuwa au kufanya kitu fulani pasipo kulazimishwa tena ukifurahia kufanya hivyo(tafsiri yangu, ruksa kuangalia Kamusi).

Nikirudi sasa MAPENZI + DHATI = MAPENZI YA DHATI: Ni mahusiano ya kimapenzi kati ya watu wawili wa jinsia tofauti ambayo yamejengwa kwa hiari ya hao watu wawili pasipo yeyote kati yao kulazimishwa tena kila mmoja ufurahia mahusiano hayo na hayuko tayali kutoka katika hayo mahusiano na angependa yaendelee milele na milele katika uhai wa maisha yao(pamoja na mapungufu ambayo mmoja wao au wote wawili watakua nayo, lakini wanafurahia kuwa pamoja na wanaelewana na kuchukuliana msingi wao ni kuwa pamoja kila mmoja akifurahia uwepo wa mwenzake).
Na haya ndio mahusiano ya watu wawili ambayo kimsingi ndio yanatakiwa yawepo ili kuhalalisha NDOA. Kama inavyoelezwa kwenye dini zetu kua ''Ndoa ni makubaliano ya watu wawili wa jinsia tofauti walioridhia kuwa pamoja katika maisha ya ndoa pasipo kusurutishwa'' na hao hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja mpaka kifo kitakapo watenganisha.

ANGALIZO:
1.Nimezungumzia Mahusiano ya Watu wawili wa jinsia tofauti maana siamini na sikubaliani na mahusiano ya watu wa jinsia moja (usagaji na ushoga)
2. Kuhusu uwepo au upatikanaji wa hayo Mapenzi ''Mie simo''
3. Kama hayo mapenzi ya dhati yakaanza kwa misingi niliyoisema hapo juu, baadae yakavunjika, ieleweke kwamba hata mapenzi ya dhati yanaweza kuvunjika yatakapopata msukosuko na wahusika wasipokua imara kuyalinda. Pia mapenzi ya dhati yanaweza jitokeza kwa watu ambao hapo awali walianza kwa mapenzi yasiyo ya dhati(kutamaniana au mazoea) na kutokana na muda na kufahamiana zaidi, wakajikuta wanaendana na hakuna anaetaka kutoka.

Hayo ni maoni yangu, waweza changaya na ya kwako ili kuboresha zaidi.

Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom