Mapenzi ni pale ambapo unaona kabisa kwamba "common sense" inapotea. Chongo unaona kengeza, lijitu liongo unaliona ni licheshi, mvivu unamwona amechoka tu, pale unapopoteza uwezo wa kuamua kwa busara. Sasa kama unayempenda naye anakupenda kwa dhati hapo ni safi sana. Tatizo ni pale unayempenda ni mbabaishaji, hapo umeula wa chuya.