Tony Yeyo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 733
- 567
Nilikutana na huyu binti nikiwa nchi za nje nasoma. Baba yake alikuwa balozi wa nchi moja ya Africa Magharibi. Huyu binti nilikutana nae akiwa na umri wa miaka 18 mimi nina 23 yaani baada ya Miaka 6 mimi wazazi wake walihama nchi yaani toka Europe kurudi Africa mana muda wao wa kustaafu ulifika.
Mimi na huyu binti tulipendana sana lakini mimi nilikataa kumuoa kwa maana niliona atapata tabu kwenda kuishi Tanzania ila Kwa upande mwingine niliona kama uzuri wake unapungua kadri muda unavyokwenda ila yeye alizidisha mapenzi yake kwangu na kila siku anataka tuongee kuhusu masuala ya ndoa.
Basi nikamwambia wewe ukifika Africa mimi nitampigia simu babako nitamueleza kwa maana familia yake wote wananitambua.
Mimi bado nikabaki Europe, alipofika Africa mimi nikabadilika nikamwambi hatuwezi kuoana. Alijaribu sana kunibembeleza nikakataa.
Tatizo nililo nalo sasa muda mwingi hunijia katika mawazo yangu namuwaza yeye, niliishi nae muda mrefu na tulizoena na najiskia vibaya kwamba nilimgeuka ila nilikuwa sina jinsi.
Wiki iliyopita kanipigia simu na kuniambia anafunga ndoa basi mpaka leo namuwaza huyu binti.Naomba Mungu anisamehe maana nilitoa ahadi ya uongo na yeye aliniamini.
Naamini atapata mpenzi mwingine na ataishi maisha mazuri . Ila kwa upande wangu sijui kama nitapata tena msichana kama yule.