Mapenzi na under 30 yamenifika haya

Mapenzi na under 30 yamenifika haya

Mgodo visa

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Posts
3,589
Reaction score
3,639
Ni kitu ambacho sikutarajia kingetokea..!

Baada ya kuvutiwa nae, na kufanya juu chini, kupata namba yake ya Simu, nilijaribu kufunguka kwa binti huyu, na (sijui Mungu au Shetani) kwa bahati nzuri nae akaelewa somo.

Tuna mawasiliano na mahusiano mazuri tu, imefikia vijana na wazee mtaani kwangu, KUNG'AMUA kinacho endelea kati yetu.

Vituko, na hiki ndicho chanzo cha kuleta Uzi huu (pengine) kwa ushauri...!

Binti kachanganyikiwa na mimi, sijui sababu, kwani ni bora ningemkuta bado ana USICHANA wake...ningesema ni mgeni wa mapenzi.

Nilikuwa na ratiba/order ya kula chakula kwa Mama nitilie, binti kaniambia nisihangaike, chakula anatoka nacho kwao...!!

Binti apungui gheto, akijua nimerudi tu kutoka katika Mishe zangu za daily....atabeba Nguo chafu na kwenda Nyumbani kwao kuzipiga SOAP...!

Kibweka kikubwa ni hiki sasa...! baada ya kubaini kuwa napendelea swala la ufugaji, najihusisha na mifugo kama Njiwa, Sungura, Bata pamoja na Kuku.

Leo hii narudi home, nimekuta ameniletea Kuku wa kienyeji wapatao 10 (kumi)

Kweli nilifurahia sana, mshangao ulikuja baadae, baada ya kugundua ameniletea MAJIKE 5 na JOGOO 5.

Nilipo mueleza umuhimu katika kuchagua kwake, angeniletea Majike angalau 8 na Madume mawili tu (nadhani kwa wafugaji wataelewa mantiki)

Kwa jibu rahisi alinijibu, "SASA HAWA WENGINE WATAPENDWA NA NANI.."?

Akimaanisha hakuna uwiano wa Majike wanne kwa Dume moja...!!

Nilimcheka...amenichukia mpaka muda huu...!!

Naombeni ushauri, nimpe somo gani..?
1b19bdab9e83793af24ea970c117a5ab.jpg

Nipo nashuhudia tu vita na ugomvi wa MAJOGOO....
 
Hajui hao ni wanyama na wanyama wana tofauti na binadamu?

Mantiki yake ya "hao watapendwa na nani" ni ya binadamu tena binadamu asyejua hata kupenda ni nini,hana sababu ya kuipeleka kwa wanyama kwasababu wanyama "hawapendani" na hawafanyi ngono kwaajili ya starehe bali kwaajili ya kuzaana na ndiyo maana jogoo mmoja anakuwa na majike manne....

Iko hivyo kwasababu kuku hapandwi kila wakati kama sisi tunavyogonoka mara nyingi hadi kulazimisha kwenye siku za period kwasababu tunachukulia ngono kama starehe wakati hao ni kinyume kabisa.....

Kufikiria wanyama wanachukulia ngono kama sisi ni kosa ambalo huyo binti amelifanya....
 
Ni kitu ambacho sikutarajia kingetokea..!

Baada ya kuvutiwa nae, na kufanya juu chini, kupata namba yake ya Simu, nilijaribu kufunguka kwa binti huyu, na (sijui Mungu au Shetani) kwa bahati nzuri nae akaelewa somo.

Tuna mawasiliano na mahusiano mazuri tu, imefikia vijana na wazee mtaani kwangu, KUNG'AMUA kinacho endelea kati yetu.

Vituko, na hiki ndicho chanzo cha kuleta Uzi huu (pengine) kwa ushauri...!

Binti kachanganyikiwa na mimi, sijui sababu, kwani ni bora ningemkuta bado ana USICHANA wake...ningesema ni mgeni wa mapenzi.

Nilikuwa na ratiba/order ya kula chakula kwa Mama nitilie, binti kaniambia nisihangaike, chakula anatoka nacho kwao...!!

Binti apungui gheto, akijua nimerudi tu kutoka katika Mishe zangu za daily....atabeba Nguo chafu na kwenda Nyumbani kwao kuzipiga SOAP...!

Kibweka kikubwa ni hiki sasa...! baada ya kubaini kuwa napendelea swala la ufugaji, najihusisha na mifugo kama Njiwa, Sungura, Bata pamoja na Kuku.

Leo hii narudi home, nimekuta ameniletea Kuku wa kienyeji wapatao 10 (kumi)

Kweli nilifurahia sana, mshangao ulikuja baadae, baada ya kugundua ameniletea MAJIKE 5 na JOGOO 5.

Nilipo mueleza umuhimu katika kuchagua kwake, angeniletea Majike angalau 8 na Madume mawili tu (nadhani kwa wafugaji wataelewa mantiki)

Kwa jibu rahisi alinijibu, "SASA HAWA WENGINE WATAPENDWA NA NANI.."?

Akimaanisha hakuna uwiano wa Majike wanne kwa Dume moja...!!

Nilimcheka...amenichukia mpaka muda huu...!!

Naombeni ushauri, nimpe somo gani..?
1b19bdab9e83793af24ea970c117a5ab.jpg

Nipo nashuhudia tu vita na ugomvi wa MAJOGOO....
Unakaa geto kisha unafuga kuku, nJiwa bata na sungura? SAWA
 
Unaonaje ukamwambia mbadilishane jogoo na mitetea kwa watu wengine
Nimejaribu kufuata ushauri wako Jose...Binti anakomaa anasema zawadi haigawiki mara mbili wala haibadirishwi kwa kitu...!!

Ila yupo anashuhudia UGOMVI tu...Manyoya yanapaa tu Angani..!!
 
Duuh hapo majanga sana...inabidi wabaki wawili majogoo ndio itafaa
 
Naona unaturingishia demu wako
Sio kama Nakuringishia Mkuu...!!
huyu mtu ni muda mfupi ila vibweka vya utoto ni vingi kuliko maelezo.

Vingine siwezi kufunguka, nawajua JF members, mtanicheka sana na kuniporomoshea Madongo.
 
Mkuu umeowa?kama hujaowa basi mke huyo Mungu kakuletea...kama anapenda kufanya mambo ya kimaendeleo kama hayo mapema hii ikiwa haijui hatma ya uhusiano wenu huoni kama ukimuweka ndani mtafika mbali zaidi kimaisha?au unatafuta mke wa picha uliyoiweka kichwani mwako?namba nane akicheka ana vidimpoz na makalio makubwa.kamatia fursa kaka haiji mara mbili hiyo.
 
Pamoja Mkuu...

Ni kweli, umri wangu nao unasogea, nafahamu kabisa umuhimu wa kuwa na mwenza, ni maisha tu hayajakaa kwenye mstari wake, Mungu akijalia, hakuna kikwazo chochote, najiandaa kwa hilo.

Asanteni sana Wadau, bibie kaelewa somo.
 
Back
Top Bottom