MAPENZI na JINO kipi kinauma Zaidi?

Mndengestani

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
931
1,000
Wana JF, jana nikiwa pande za Beach na madada nikawasikia wanasema eti MAPENZI yanauma, sasa kila nikifikiria sipati jibu. Haya mapenzi yanauma vipi.

Kwakua nilishawai kuumwa jino basi haraka nikafananisha kama maumivu ya JINO. Sasa sijui kati ya JINO na MAPENZI kipi kinauma zaidi.

Naombe sana kwa anayejua
 

SK2016

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,693
2,000
Jino linauma mbayaaa ila likipata dawa au liking'olewa vizuri maumivu yanatokomea kabisa. Lakini maumivu ya mapenzi hata ukiyapatia suluhisho bado yataendelea kukutesa. Maumivu hayo huisha polepole mno na usipopata replacement yake ya ukweli, utaendelea kuumia.
Ni hayo tu.
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,261
2,000
si kila aliyepata maumivu ya jino umeumizwa/jeruhiwa na mapenzi na wengi wanaumizwa na mapenzi bila kukumbana na kadhia za meno.

Kikubwa vyote vinatibika na mtu huweza kuendelea na maisha yake hata akasahau maumivu aliyopata kukumbana nayo.
 

Thad

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
12,423
2,000
Maumivu ya mapenzi hayana dawa..............kuna aliyewahi kujiua kwa ajili ya maumivu ya jino?
 
Top Bottom